Kufutwa kwa baadhi ya vipengele katika sheria ya kuondoka katika maeneo hayo ya awali itawaruhusu wakazi wa Kiyahudi kurejea katika maeneo manne ya makazi huko Ukingo wa Magharibi waliamriwa kuhama mwaka 2005 kwa sharti la kuidhinishwa na jeshi la Israeli.
Yuli Edelstein, mkuu wa Kamati ya Mambo ya Nje na Ulinzi katika Bunge la Israeli, amepongeza hatua hiyo ikiwa “ hatua ya kwanza na muhimu katika kurekebisha na kuimarisha taifa la Israeli katika maeneo hayo ya ndani ya nchi ambayo ni mali yake.
Tangu vita vya mwaka 1967, Israeli imeunda kiasi cha makazi 140 katika ardhi Wapalestina wanaiona ni sehemu kuu ya mustakbali wa taifa lao, ambapo zaidi ya walowezi 500,000 wanaishi hivi sasa. Mbali na makazi hayo yaliyoidhinishwa, makundi ya walowezi wamejenga vituo kadhaa bila ya kibali cha serikali.
Mataifa mengi yaliyo na nguvu duniani yanachukulia ujenzi wa makazi hayo katika maeneo yaliyokamatwa na Israeli katika vita vya mwaka 1967 ni kinyume cha sheria za kimataifa na upanuzi wake ni kikwazo kwa amani, kutokana na kuchukua ardhi ambayo Wapalestina wanadai katika siku za usoni itakuwa taifa lao.
Kura hiyo ya bunge, ikiwa ni moja ya hatua kuu za mwanzoni zilizochukuliwa na muungano wa mrengo wa kulia wenye msimamo mkali wa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, umekuja siku kadhaa baada ya maafisa wa Israeli na Palestina kukubaliana katika hatua za kuzuia ghasia na uchochezi huku mivutano ikisambaa.
Mamlaka yaPalestina mara moja ililaani uamuzi huo.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters.