Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 10:06

Kurejeshwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Saudi Arabia na Iran ni changamoto kwa Israel - Wachambuzi


Mpatanishi Wang Yi (Katikati), Ali Shamkhani na Musaad bin Mohammed Al Aiban wakutana mjini Beijing.
Mpatanishi Wang Yi (Katikati), Ali Shamkhani na Musaad bin Mohammed Al Aiban wakutana mjini Beijing.

Hatua ambayo haikutarajiwa na wengi ya Saudi Arabia kurejesha uhusiano na Iran inaongeza changamoto mpya ya kidiplomasia kati ya Saudi Arabia na Israeli, ambayo pia ilitumai kwamba uhusiano kati yake na Saudia ungeimarika, wachambuzi wanasema.

Riyadh na Tehran zilitangaza siku ya Ijumaa kwamba baada ya miaka saba ya kusitishwa kwa uhusiano, watafungua tena ubalozi ndani ya miezi miwili na kutekeleza makubaliano ya usalama na ushirikiano wa kiuchumi yaliyotiwa saini zaidi ya miaka 20 iliyopita.

Makubaliano hayo yaliyoongozwa na China yaliibua ukosoaji mkali ndani ya Israeli, chini ya uongozi wa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, ambaye ameweka wazi azima yake ya kuileta Saudi Arabia kwenye Saudia kwenye meza ya mazungumzo kama sehemu ya muungano wa kikanda dhidi ya Iran.

Kiongozi wa upinzani wa Israel Yair Lapid alisema inawakilisha "hatari na kushindwa kabisa kwa sera ya kigeni ya serikali ya Israeli".

Hata hivyo waangalizi wa kikanda walitahadharisha kwamba athari halisi za makubaliano hayo haziko wazi -- katika suala la ushirikiano wa baadaye wa Saudi-Iran na uhusiano wa Israel na Riyadh.

Dhana kwamba Saudi Arabia ilikuwa na nia ya kipekee kwa Israel kama sehemu ya uwezekano wa kukabiliana na Iran daima ilikuwa "ya juujuu", alisema mchambuzi wa Saudi Aziz Alghashian.

Saudi Arabia, nyumbani kwa maeneo matakatifu zaidi ya Uislamu huko Mecca na Madina, kwa muda mrefu imesema kuitambua Israel kunategemea suluhisho la mataifa mawili na Wapalestina.

Haikujiunga na Mkataba wa Abraham wa 2020 ulioidhinishwa na Marekani ambao ulishuhudia taifa la Kiyahudi likianzisha uhusiano na majirani wawili wa ufalme huo, Umoja wa Falme za Kiarabu na Bahrain.

Makubaliano mapya ya Saudi-Iran "yanaweza kusababisha pengo kubwa kati ya Israel na Saudi Arabia ikiwa hii itatoa fursa pana ya kidiplomasia kati ya ufalme huo na Iran", alisema Brian Katulis wa Taasisi ya Mashariki ya Kati huko Washington.

"Israel ina mashaka na diplomasia yoyote na utawala wa Tehran," aliongeza

Hilo linaufanya mkataba wa Saudi-Iran kuwa "ushindi wa wazi wa kidiplomasia kwa Iran" na "pigo" kwa Netanyahu, alisema Nicholas Heras wa Taasisi ya New Lines ya Mikakati na Sera.

"Saudi Arabia, ambayo inaandamwa sana na Israel, ilituma ishara kubwa kwa serikali ya sasa ya Israeli kwamba Waisraeli hawawezi kutegemea Riyadh kuunga mkono hatua za kijeshi za Israel dhidi ya Iran, popote pale katika eneo," alisema.

Sio kila mtu anafikiria kuwa matokeo ni dhahiri sana, hata hivyo.

XS
SM
MD
LG