Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:07

Afghanistan:Taliban waahidi kulegeza marufuku ya elimu kwa wanawake


Wanafunzi wanawake wa Afghanistan wakisimama nje ya Chuo kikuu cha mjini Kabul, Disemba 21, 2022. Picha ya AP
Wanafunzi wanawake wa Afghanistan wakisimama nje ya Chuo kikuu cha mjini Kabul, Disemba 21, 2022. Picha ya AP

Taliban wanaoongoza nchini Afghanistan Alhamisi wameeleza kuwa wanaweza kulegeza marufuku ya elimu kwa wanawake, wakisema kazi inafanyika kusahihisha “hatua hiyo ya muda”.

Taarifa hiyo imetokea kama jibu kwa wito wa muungano wa nchini nyingi za Kiislamu kwa kundi hilo la Kiislamu kubalitisha marufuku yake ya elimu kwa wasichana na wanawake kufanya kazi kwenye mashirika ya misaada.

Shirika hilo lenye nchi wanachama 57, au OIC, lenye makao yake Saudi Arabia, liliitisha “mkutano wa dharura” wa kamati yake ya utendaji Jumatano ili kujadili vikwazo vya Taliban dhidi ya wanawake.

Taarifa ya OIC baada ya mkutano huo ilielezea marufuku hiyo kama ukiukaji wa sheria za Kiislamu na “ mbinu ya Mtume Muhammad, ikiwataka Taliban kufikiria upya maamuzi ya kuwapiga marufuku wanawake kupata elimu na kazi.

OIC imelezea maskitiko yake juu ya kusitisha elimu kwa wanawake nchini Afghanistan na uamuzi wa kuamuru mashirika yote ya kitaifa na kimataifa yasiyo ya kiserikali kuwasimamisha kazi wafanyakazi wa kike hadi itakapotangazwa hatua nyingine, ilisema katika taarifa.

XS
SM
MD
LG