Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 15:44

Saudi Arabia yasisitiza uungaji mkono wake kwa Ukraine


Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akizungumza na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz mjini Kyiv, Ukraine Januari 25, 2023.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akizungumza na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz mjini Kyiv, Ukraine Januari 25, 2023.

Saudi Arabia ilisisitiza uungaji mkono wake kwa Ukraine wakati wa ziara ya waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo mjini Kyiv siku ya Jumapili.

Prince Faisal bin Farhan Al Saud alikutana na Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskiy ambaye aliishukuru Saudi Arabia kwa ushirikiano na kuipatia misaada.

Ukraine na Saudi Arabia walianza uhusiano wa kidiplomasia mwaka 1993.

“Nina furaha kwamba leo tunaikaribisha nchi yako. kwa kweli ni muhimu sana kwetu, Nijuavyo, kwa mara ya kwanza katika miaka 30, zaidi ya miaka 30 ya uhuru wetu. Kwa hiyo unakaribishwa sana.” Zelenskiy alisema katika mkutano wake na ujumbe huo mjini Kyiv.

Mwezi Oktoba, Saudi Arabia ilisema itatoa dola milioni 400 za misaada ya kibinadamu kwa Ukraine na kuelezea utayari wa ufalme huo kuendelea na juhudi za upatanishi na kuunga mkono kila kitu kinachochangia kupunguza mivutano, Shirika la Habari la Serikali la Saudi -SPA lilisema.

Mwezi Septemba, Saudi Arabia ilipata ushindi wa kidiplomasia kwa kuachiliwa huru wapiganaji wa kigeni waliotekwa nchini Ukraine.

Kwa upatanishi wa Mwana Mfalme Mohammed bin Salman, Russia Septemba 2022 iliwaachilia wageni 10 iliyokuwa imewakamata nchini Ukraine, wakiwemo Waingereza watano na Wamarekani wawili.

XS
SM
MD
LG