Nchi zote mbili zimetetea mpango huo, ambao unataka Uingereza kuhamisha wakimbizi walioko nchini kwake kwenda Rwanda.
Viongozi hao wawili wamepongeza ushirikiano wao wa uhamiaji na maendeleo ya kiuchumi ambayo yanakabiliana na usafirishaji hatari wa binadamu na kutoa fursa kujenga maisha mapya katika nchi salama, ofisi ya Johnson imesema hayo.
Mkutano wao pembeni ya mkutano wa Jumuiya ya Madola unafuatiwa na mazungumzo mjini Kigali Jumatano baina ya Kagame na Mwanamfalme wa Uingereza Charles ambaye aliripotiwa akisema kuwa mpango huo unasikitisha.
Makundi ya kutetea haki za binadamu, viongozi wa kanisa na Umoja wa Mataifa pia wamepinga mpango huo ambao ulitishia kugubika mkutano wa viongozi wa serikali wa Jumuiya ya Madola.