Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 07:02

DRC yafunga mipaka yake yote na Rwanda


Ramani ya nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Rwanda na DRC.
Ramani ya nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Rwanda na DRC.

Serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imefunga mipaka yake yote na Rwanda huku hali ya miwavutano kati ya nchi hizo mbili ikiendelea kuongezeka kufuatia madai ya Rwanda kuunga mkono waasi wa M23 wanaopigana na jeshi la Congo.

Mpaka wa Petit Barier ulio mjini Goma, utakuwa ukifungwa kuanzia saa tisa alasiri hadi saa moja asubuhi ili kuruhusu wafanyabiashara kufanya shughuli zao.

Awali, mwanajeshi wa DRC alivuka mpaka na kuingia Rwanda ambapo aliwashambulia kwa risasi na kuwajeruhi polisi wawili wa Rwanda kabla ya mwanajeshi huyo kupigwa risasi na kuuawa.

Wakati huo huo, Kundi la wapiganaji wa M23 wamepiga risasi na kuitungua ndege ya jeshi la DRC karibu na mji wa Goma. Msemaji wa waasi hao Majro Willy Ngoma amemwambia mwandishi wa Sauti ya Amerika mjini Goma kwamba waliiangusha ndege hiyo kwa sababu ilikuwa imeingia katika ngome zao kwa lengo la kuwashambulia.

Hakuna taarifa kuhusu vifo wala majeruhi kufikia sasa.

XS
SM
MD
LG