Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 15:28

Rais Kenyatta aomba jeshi la Afrika mashariki lipelekwe DRC

Rais Uhuru Kenyatta na Rais wa DRC Felix Tshisekedi wakikumbatiana baada ya kusainiwa mkataba unaoiruhusu DRC kuwa mwanachama wa EAC, Nairobi, April 8, 2022. Picha ya AFP
Rais Uhuru Kenyatta na Rais wa DRC Felix Tshisekedi wakikumbatiana baada ya kusainiwa mkataba unaoiruhusu DRC kuwa mwanachama wa EAC, Nairobi, April 8, 2022. Picha ya AFP

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta Jumatano aliomba kikosi cha kanda ya Afrika mashariki kipelekwe katika eneo la Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo lenye mzozo ili kurejesha usalama mashariki mwa nchi hiyo, ambako mapigano makali ya hivi karibuni yamezusha tena uhasama wa zamani.

Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, nchi yenye utajiri wa madini inasumbuka kudhibiti darzeni ya makundi yenye silaha mashariki mwa taifa hilo kubwa, ambayo mengi kati yao ni urithi wa vita viwili vya kikanda robo karne iliyopita.

Ghasia za wiki kadhaa zimechochea mvutano wa kidiplomasia kati ya DRC na jirani yake Rwanda, DRC ikiishtumu Rwanda kwa uasi wa hivi karibuni wa kundi la waasi wa M23 ulioibuka tena.

Rwanda ilikanusha mara kadhaa kwamba haiwasaidii waasi hao, huku nchi hizo mbili kila moja ikiishtumu nyingine kuendesha mashambulizi ya makombora ya kuvuka mpaka.

"Natoa wito wa kuanzishwa kwa jeshi la Afrika mashariki chini ya usimamizi wa Jumuia ya Afrika mashariki,", Kenyatta amesema katika taarifa.

Ameongeza kuwa "uhasama uliopo" umetishia kukwamisha mchakato wa kisiasa unaoendelea kushughulikia hali ya usalama katika nchi hiyo yenye raia milioni 90.

Uamuzi wa kuunda kikosi cha kikanda ulichukuliwa mwezi Aprili wakati Kenyatta alikuwa mwenyeji wa viongozi wa Uganda, Burundi, Rwanda na DRC mjini Nairobi kujadili mzozo wa DRC.

Makamanda wa kijeshi wa nchi saba wanachama wa Jumuia ya Afrika mashariki watakutaka Jumapili kukamilisha maandalizi ya kupeleka kikosi hicho cha mseto, Kenyatta amesema.

"Jeshi la kanda ya Afrika mashariki litapelekwa katika majimbo ya Ituri, Kivu Kaskazini na Kivu Kusini mara moja kuleta utulivu katika eneo hilo na kuimarisha amani."

XS
SM
MD
LG