Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 06:31

Ruto na Raisi wa Iran washindwa kukutana na waandishi wa habari Kenya


Rais wa Iran Ebrahim Raisi alipomkaribisha rais wa Belarus Alexander Lukashenko Tehran, Machi 13, 2023. Picha na Tovuti ya rais wa Iran/WANA/ REUTERS.
Rais wa Iran Ebrahim Raisi alipomkaribisha rais wa Belarus Alexander Lukashenko Tehran, Machi 13, 2023. Picha na Tovuti ya rais wa Iran/WANA/ REUTERS.

Rais wa Iran Ebrahim Raisi, ambaye alitarajiwa kuanza ziara nchini Kenya siku ya Jumanne, kwa sasa ataanza ziara hiyo siku moja baadaye, wizara ya mambo ya nje ya Kenya ilisema baada ya rais huyo kushindwa kushiriki katika hafla na waandishi wa habari.

Ziara hiyo ya nadra kwa Kenya, Uganda na Zimbabwe inaashiria juhudi za hivi karibuni za kidiplomasia za Jamhuri ya Kiislamu zakuskuma muungano mpya na kupunguza kutengwa kwake kimataifa.

Ziara hiyo ya siku tatu itakuwa ya kwanza kwa rais wa Iran barani Afrika katika kipindi cha miaka 11.

Rais Raisi awali alitarajiwa kuwa pamoja na rais William Ruto wa Kenya, katika mkutano na waandishi wa habari Jumanne asubuhi, lakini hakuna hata mmoja kati yao aliyejitokeza.

"Ratiba ya rais sasa imepitiwa upya ili kuruhusu kukamilishwa kwa makubaliano muhimu (memoranda of understanding) ambayo ni muhimu katika kuendeleza uhusiano," wizara ya mambo ya nje ya Kenya ilisema katika taarifa.

"Rais wa Iran sasa atawasili kesho kwa ziara ya kiserikali."

Kulingana na shirika rasmi la habari la IRNA la Iran, Raisi ataongoza ujumbe unaomjumuisha waziri wa mambo ya nje pamoja na wafanyabiashara wakubwa. Amepangiwa kukutana na marais kutoka nchi tatu za Afrika.

Siku ya Jumatatu, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Nasser Kanani alielezea safari hiyo kama "mwelekeo mpya" ambao unaweza kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya Iran na nchi za Afrika.

Pia msemaji huyo wa wizara ya mambo ya nje ya Irani alisema maelewano hayo yanatokana na "msimamo inayofanana ya kisiasa” kati ya Tehran na nchi hizo tatu za Kiafrika.
Iran imezidisha juhudi zake za kidiplomasia katika miezi ya karibuni ili kupunguza hali ya kutengwa kwake na kumaliza athari za vikwazo vikali ilivyowekewa tena, tangu kujiondoa kwa Marekani katika mashauriano ya nyuklia mwaka 2018.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG