Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 02:18

Mahakama ya Rufaa Iran imemhukumu mwanaharakati miaka mitano jela


Golrokh Ebrahimi Iraee (USCIRF)
Golrokh Ebrahimi Iraee (USCIRF)

Iraee alikataa kushiriki katika usikilizwaji wa kesi yake kwenye mahakama ya rufaa akishutumiwa kushiriki katika mikusanyiko haramu na kukiuka usalama wa taifa, akisema hakutambua uhalali wa mahakama hiyo, makundi ya haki za binadamu yanasema

Mahakama ya rufaa nchini Iran imemhukumu kifungo cha miaka mitano mwanaharakati maarufu na mwandishi wa habari Golrokh Iraee ambaye amekuwa akizuiliwa tangu kukamatwa kwake mwanzoni mwa vuguvugu la maandamano, wafuasi wake wamesema siku ya Jumapili.

Iraee alikataa kushiriki katika usikilizwaji wa kesi yake kwenye mahakama ya rufaa akishutumiwa kushiriki katika mikusanyiko haramu na kukiuka usalama wa taifa, akisema hakutambua uhalali wa mahakama hiyo, makundi ya haki za binadamu yanasema.

Alikamatwa Septemba mwaka jana katika msako wa polisi akiwa nyumbani kwake mwanzoni mwa vuguvugu la maandamano yaliyochochewa na kifo cha Mahsa Amini, ambaye alikuwa amezuiliwa kwa madai ya kukiuka sheria kali za mavazi kwa wanawake.

Golrokh Iraee, ambaye alikuwa katika gereza la Evin kwa siku 280 alihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela na mahakama ya Tehran kulingana na akaunti ya Twitter iliyopo kwa jina lake inayoendeshwa na wafuasi wake.

Mahakama ya mwanzo ilimhukumu kifungo cha miaka saba mwezi Aprili.

Anajulikana kwa kampeni zake juu ya masuala kadhaa ikiwa ni pamoja na hukumu za kupigwa mawe na hali ya jela, Iraee ni mke wa mwanaharakati Arash Sadeghi, ambaye pia alikamatwa wakati wa harakati za maandamano lakini sasa ameachiliwa.

Baadhi ya wanaharakati waliokamatwa wakati wa ukandamizaji wa Iran dhidi ya vuguvugu la maandamano wameachiwa huru katika miezi michache iliyopita wakati maandamano hayo yakizidi kuongezeka.

Lakini wapiga kampeni maarufu wanawake, bado wako gerezani ikiwa ni pamoja na mshindi wa tuzo, Narges Mohammadi, mwanaharakati wa haki za ajira, Sepideh Gholian pamoja na waendesha kampeni za mazingira Niloufar Bayani na Sepideh Kashani.

Wakati huo huo, waandishi wawili wanawake ambao walifanya mengi kufichua kesi ya Amini, Niloufar Hamedi na Elaheh Mohammadi, ambao pia wanashikiliwa tangu Septemba wanashikiliwa mjini Tehran kwa mashtaka ya usalama wa taifa.

Forum

XS
SM
MD
LG