Kifo cha Mahsa Amini mwenye umri wa miaka 22 mwezi Septemba mwaka wa 2022 akiwa chini ya ulinzi wa polisi wa maadili, kilichochea wimbi la maandamano makubwa kote Iran, na kuashiria changamoto kubwa kwa viongozi wake wa kidini katika kipindi cha miongo kadhaa.
Tangu wakati huo, watu kadhaa walinyongwa kwa kushiriki katika maandamano, viongozi wa Iran wakizishtumu nchi adui za magharibi kuchochea maandamano hayo.
“Tunawaomba Viongozi wa Iran kusitisha hukumu ya kunyongwa kwa watu waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kifo kuhusiana na maandamano na kusisitiza maombi yetu ya kupewa nyaraka za mahakama, ushahidi na hukumu kuhusu kila mmoja wa watu hawa,” Sara Hossain, mwenyekiti wa tume ya kutafuta ukweli kuhusu Iran, ameliambia Baraza la Umoja wa mataifa la haki za binadamu mjini Geneva.
Tume hiyo imetoa pia wito wa kuachiliwa kwa wale waliokamatwa kwa kutumia haki yao halali ya kukusanyika kwa amani na kuripoti maandamano.”
Forum