Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 23:37

Russia yaendelea kujenga uhusiano imara na Afrika, uwepo wake wa kijeshi waongozeka


Ishara mpya ya uwepo wa Russia Afrika yaonekana Burkina Faso
please wait

No media source currently available

0:00 0:05:44 0:00

Ishara mpya ya uwepo wa Russia Afrika yaonekana Burkina Faso

Russia imeifanya dunia iifuatilie kutokana na msimamo wake wa kichokozi dhidi ya Ukraine.

Uliokuwa utawala wa umoja wa kisovieti umekuwa ukijenga mahusiano na Afrika kwa ukimya zaidi, ikimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kijeshi, lakini pia ikiongeza wasi wasi kwa mataifa ya Magharibi kuhusu mbinu na malengo yake huko.

Bendera za Russia zilipepea katika mji mkuu wa Burkina Faso kufuatia mapinduzi ya kijeshi ya Januari katika taifa la Afrika Magharibi. Sanamu moja ilizinduliwa huko Jamhuri ya Afrika ya Kati mwaka uliopita ikionyesha wanajeshi wa nchi hiyo, wakiungwa mkono na wapiganaji wa Russia, wakiwalinda raia.

Hizo ni alama za wazi zaidi za uwepo wa kijeshi wa Russia katika bara hilo. Afrika ni kipaumbele katika sera yake ya mambo ya nje, Rais wa Russia Vladimir Putin alisema katika mkutano wa kwanza kati ya Russia na Afrika wa viongozi wa kisiasa na biashara mwaka 2019.

“Hatutashiriki katika “mgao” mpya wa utajiri wa bara hilo,” alisema. Badala yake, tuko tayari kujihusisha na ushindani kwa kushirikiana na Afrika.”

Mkutano wa St. Petersburg

Mkutano wa pili umepangwa kufanyika St. Petersburg mwezi Oktoba. Mkutano wa kwanza, katika mji wa mapumziko wa Sochi huko Black Sea, ulipelekea mikataba ya kidiplomasia na makubaliano ya mabilioni ya dola inayohusu silaha, nishati, kilimo, benki na mengineyo, alisema muandaaji huyo, ambayo ni taasisi ya Roscongress.

Moscow imekuwa ikijenga mahusiano mapya na kurejesha ushirikiano uliokuwepo enzi ya Vita Baridi, wakati ilipokuwa Umoja wa Sovieti ilipounga mkono harakati za kisoshalisti kote Afrika. Baada ya kuvunjika muungano huo mwaka 1991, kwa kiwango kikubwa ilijiondoa katika bara hilo.

Tangu angalau mwaka 2007, hasa katika miaka michache iliyopita, Russia imeongeza kujihusisha kwake kijeshi na kiuchumi barani Afrika. Mkutano wa mwaka 2019 ulipelekea kuwepo mikataba na zaidi ya nchi 30 za Afrika kuwapatia silaha na vifaa vya kijeshi, wamewekeza kwa kiwango kikubwa katika sekta ya usalama, teknolojia na viwanda vinavyochimba mali ghafi kama vile mafuta, gesi, dhahabu na madini mengine.

Rusal ni kampuni ambayo inachimba madini ya aluminium huko Guinea na kikundi cha nyuklia Rosatom inayotafuta uranium nchini Namibia. Alrosa, ni kampuni kubwa zaidi duniani inayochimba almasi, imepanua operesheni zake Angola na Zimbabwe, kulingana na Carnegie Endowment for International Peace.

“Ni wazi Russia ina maslahi, ikitafuta masoko mapya ya kiuchumi na ushawishi wa kisiasa huko Afrika,” amesema Tatiana Smirnova, mtafiti wa shahada ya uzamivu katika Kituo cha FrancoPaix ya Chuo Kikuu cha Quebec na mshiriki katika Kikundi cha Watafiti wa Sahel wa Chuo Kikuu cha Florida. “Ni muhimu kwa Russia.”

Biashara kati ya Russia na Nchi za Afrika

Biashara kati ya Russia na nchi za Afrika imeongezeka maradufu tangu mwaka 2015, kufikia karibu dola bilioni 20 kwa mwaka, Rais wa Afrika wa Import-Export Bank, Benedict Oramah amesema katika mahojiano mwaka jana na shirika la habari la Tass linalomilikiwa na serikali ya Russia, iliyoelezwa na tovuti ya ya habari la Russia Briefing. Amesema Russia ilisafirisha nje ya nchi bidhaa na huduma zenye thamani dola bilioni 14 na kuingiza nchini takriban bidhaa za Afrika za dola bilioni 5.

Ramani ya Afrika
Ramani ya Afrika

Hata hivyo, Afrika inafanya biashara zaidi na nchi nyingine, haswa China, ni mshirika wake mkubwa zaidi katika miaka ya hivi karibuni.

Msimamo wa Russia katika miaka ya karibuni ni ushirikiano usiokuwa na masharti ya kisiasa au mengine” yanayowekwa na nchi za Magharibi, Putin amesema.

“Russia inatoa, kama ilivyokuwa ikifanya hapo kabla kwa Umoja Sovieti, mtizamo mbadala kwa mataifa ya Afrika” kulingana na “Ukosoaji huu maarufu dhidi ya Magharibi,” amesema Maxim Matusevich, profesa wa historia anayeongoza utafiti wa Russia katika Chuo Kikuu cha Seton Hall huko New Jersey.

Hata hivyo. Wakati Soviet ilijaribu kuuza fikra za kisoshalisti za kuiendeleza Afrika, Russia leo “ hawatoi itikadi yoyote yenye dira,” amesema. “Kitu muhimu wanachofanya ni kufikia makubaliano na matajiri mmoja mmoja wa Afrika. … Wanasisitiza juu ya umuhimu wa uhuru na kulinganisha na nchi za Magharibi, ambapo wanajaribu kulazimisha maadili yao, kama vile uwazi, serikali zenye ukweli, sheria za kupambana na ufisadi. Na tena, siyo kwamba nasema nchi za Magharibi siku zote ni wakweli katika hilo, lakini huo ndio ujumbe wao rasmi – na wao [Russia] hawafanyi chochote katika hilo.”

Jeshi la Russia lachukua fursa kuongeza uwepo wake

Kuenea kwa wanamgambo wenye itikadi kali za Kiislam na aina nyingine za vurugu katika Afrika kumefungua fursa nyingi kwa jeshi la Russia kujihusisha. Kwa mfano, nchi tano katika eneo la Sahel lenye vita – Burkina Faso, Chad, Mali, Mauritania na Niger – ziliomba msaada wa kijeshi wa Moscow mwaka 2018. Wapiganaji wa Russia pia wameombwa kusaidia huko Msumbiji na Angola.

Mpango wa Ufaransa kuondoa majeshi yake kutoka Mali, koloni lake la zamani na mshirika katika mapambano dhidi ya wanajihadi tangu 2013, inatoa fursa zaidi.

Alhamisi iliyopita, Ufaransa na washirika wake wa usalama walitangaza wataondoka Mali, “wakieleza kuingiliwa kati” utawala wa kijeshi tangu walipochukua madaraka mwaka 2020. Ufaransa inapeleka wanajeshi wake 2,400 kwingineko huko Sahel.

Wakandarasi binafsi wa kijeshi pia wanasaidia kusukuma mbele ajenda za Moscow barani Afrika, wafuatiliaji wa Magharibi wanasema. Hawa ni pamoja na wapiganaji wa kikundi cha Wagner Group, kinachodaiwa kudhibitiwa na Yevgeny Prigozhin mshirika wa Putin. Putin amekanusha kuwa na mahusiano yoyote na kikundi hicho.

“Siyo serikali,” Putin amesema. “… Ni biashara binafsi yenye maslahi binafsi ikijihusisha na uchimbaji wa rasilimali za asili za nishati, ikwemo rasilimali kama dhahabu au vito vya thamani.

Rais wa Russia Vladimir Putin
Rais wa Russia Vladimir Putin

Hao wapiganaji binafsi wanafanya shughuli zao sambamba na Kremlin, amesema Joseph Siegle, anayeongoza utafiti katika Kituo cha Afrika cha Masuala ya Mkakati, sehemu ya Wizara ya Ulinzi ya Marekani. Amesema hao ni sehemu ya vitendea kazi vya Moscow kuwaondoa viongozi dhaifu wa Kiafrika kwa mabadilishano ya kiuchumi na maslahi mengine.

“Kila mahali tumeona Wagner wamepelekwa duniani kote na huko Afrika – iwe ni Libya, Sudan, Msumbiji, Jamhuri ya Afrika ya Kati – imekuwa ni jeshi la kuzidhoofisha nchi,” Siegle alisema. “Kile ambacho Russia imekuwa ikifanya ni kupeleka mamluki, kusambaza habari potofu, kuingilia uchaguzi, kubadilishana silaha kwa mali ghafi, mikataba ya opaque … yenye lengo la kueneza ushawishi wake eneo kubwa.

Ushawishi huo unaweza kulinda maslahi ya Russia katika duru za kimataifa, Matusevich alisema, akieleza jinsi Russia ilivyoiteka Rasi ya Crimean mwaka 2014.

“Tunajua kuwa katika uovu uliotokea katika uvamizi wa Ukraine, wakati Russia ilipowekewa vikwazo katika Umoja wa Mataifa, mataifa mengi ya Afrika walisita kupiga kura,” amesema. “Kwa hiyo, wao wanapata kuungwa mkono kidiplomasia na makundi ya kidiplomasia mbadala ambayo wanaweza kuyategemea.

Umoja wa Mataifa unafanyia uchunguzi ripoti za ukiukwaji “mkubwa” wa haki za binadamu huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, uliotendwa na wanajeshi binafsi. Wakati huo huo, mamluki wa Russia wanapongezwa kama walinzi wa umma katikati ya jaribio la mapinduzi katika filamu ya Russia 2021 The Tourist. Filamu hiyo, iliyotengenezwa huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, inaripotiwa kufadhiliwa na Pregizhin, mshirika wa Putin.

Security concerns

Nchini Mali, viongozi wa mapinduzi ya kijeshi ya 2020 waliwaleta wakufunzi wa kijeshi wa Russia – na kile ambacho mamlaka za Marekani na Ufaransa zinasema ni mamluki wa Wagner.

Baadhi huko Mali waliwakaribisha mamluki haa kwa kupeperusha bendera za Russia, siyo tu wakionyesha mahusiano ya kihistoria na iliyokuwa USSR lakini pia kutoweka kwa ustahmilivu wa umma kwa kuendelea kwa ukosefu wa usalama, amesema Niagale Bagayoko, mwanasayansi mwenye makazi yake Paris anayeongoza mtandao wa sekta ya usalama ya Africa.

Taasisi hiyo inataka kuwepo mageuzi ya kiusalama na haki, na ni kati ya wanaotetea kuwepo ulinzi zaidi kwa raia katika eneo la Sahel na uwazi zaidi na uwajibikaji kwa operesheni za kijeshi huko.

“Mwaka 2013, watu wote wa Mali [walikuwa] wanashauku walipowasili Wafaransa … leo hawataki uwepo wao,” Bagayoko amesema.

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa
Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa

“Kusema kweli, sishangazwi sana iwapo, katika miaka miwili au zaidi, hilo linaweza kutokea kwa uwepo wa Russia,” amesema.

Nchi za Afrika zinaonyesha utayari wao kuangalia kuwa na zaidi ya mshirika mmoja katika juhudi za kutafuta utulivu na usalama, alisema. “Kuna kutambua hilo…kuwa na ushirika na watendaji wa upande moja … ni kuzuia uwezekano wa diplomasia kufanyika, na pia vifaa mbalimbali vya kijeshi.”

Russia siyo serikali ya kigeni pekee inayojaribu kueneza ushawishi wake Afrika, ambako kuna rasilmali nyingi ikiwemo idadi inayoongezeka ya vijana.

White House inapanga mkutano wa pili wa viongozi wa Marekani na Afrika baadae mwaka huu, unaofuatia mkusanyiko wa awali uliofanyika Washington mwaka 2014 na Umoja wa Ulaya imetangaza uwekezaji mpya wa dola milioni 172 katika miundombinu, kukabiliana na juhudi za mradi wa miundombinu maarufu kama Belt and Road Initiative wa China.

XS
SM
MD
LG