Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 15:16

Jumuiya ya Kimataifa yalaani uvamizi wa Rashia mashariki ya Ukraine


Waandamanaji nje ya Wizara ya mambo ya nje mjini Kiyv wakiomba Umoja wa Ulaya kuongeza vikwazo dhidi ya Rashia.
Waandamanaji nje ya Wizara ya mambo ya nje mjini Kiyv wakiomba Umoja wa Ulaya kuongeza vikwazo dhidi ya Rashia.

Rais wa Ukraine anatoa wito kwa mataifa ya dunia kuiweka Rashia vikwazo vikali zaidi hivi sasa kabla ya Moscow kuendelea na uvamizi wake.

Mataifa ya Ulaya na Marekani yameanza kutangaza vikwazo dhidi ya Rashia baada ya Rais Valdimir Putin kutambua uhuru wa Jamhuri mbili za Ukraine na kuamrisha wanajeshi wake kuingia katika majimbo hayo.

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amekua kiongozi wa kwanza wa nchi za magharibi kuchukua hatua dhidi ya Rashia kwa kuzia kuidhinishwa mradi muhimu wa bomba la kusafirisha gesi ghafi kutoka Rashia hadi Ujerumani, inayofahamika kama “Nord Stream 2.”

Kiongozi huyo amechukua hatua hiyo katika kujibu uwamuzi wa Moscow kupeleka wanajeshi wake mashariki ya Ukriane usiku wa Jumatatu Februari 21, 2022.

Akizungumza na waandishi habari akiwa pamoja na mgeni wake waziri mkuu wa Ireland, Micheal Martin, Kansela Scholz alitoa wito wa kuendelea na juhudi za kidiplomasia wanapotangaza vikwazo vipya.

“Kaika awamu hii, ni muhimu na inabidi kwa hivi sasa kuzuia kuzorota zaidi kwa mvutano na kupelekea kutokea kwa janga kamili, mbali na vikwazo vya awali, hiyo ikiwa ni lengo la juhudi zetu zote za kidiplomasia. Hizi ni siku na saa ngumu sana kwa Ulaya, karibu miaka 80 baada ya kumalizika kwa vita vya pili vya dunia, kwa vile kuna kitisho cha kutokea tena vita mashariki ya Ulaya. Ni jukumu letu kuepusha janga kama hilo kutokea. Na kwa mara nyingine tena nina toa wito kwa Rashia kusaidia,” alisema Scholz.

White House imepongeza hatua ya Ujerumani kusitisha mradi wa Nord Stream 2. Msemaji wa Ikulu Jen Psaki amesema kwamba “Rais Joe Biden aliweka bayana kwamba atashirikiana na Ujerumani kuzuia mradi huo ikiwa Rashia itaivamia Ukraine.”

Na Jumanne White House imetangaza kwamba kitendo cha Rashia cha kutambua Jamhuri za Dinetsk na Lugansk kua ni huru na kupelekea wanajeshi wake huko, ni mwanzo wa uvamizi wa Ukraine.

Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson akitangaza vikwazo vya nchi yake akiwa bungeni siku ya Jumanne, amesema wanawekea vikwazo mabenki matano na matajiri wawili wakuu wa Rashia, aliongeza kusem huu ndio mwanzo wa kuchukuliwa hatua thabiti dhidi ya Rashia.

“Hivi sasa Uingereza na washirika wake wanaanza kuiwekea Rashia vikwazo ambavyo tumetayarisha kuchukua, kwa kutumia mamlaka mpya na ambayo hayajawahi kutumika yaliyoidhinishwa na baraza hili la bunge, kuwawekea vikwazo wa-Rasia na vyombo vyenye umuhimu mkubwa kimkakati kwa Kremlin,” alisema Johnson.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, ameeleza wasi wasi wake mkubwa kutokana na uwamuzi wa Rashia kuingia huko mashariki mwa Ukraine. Katika taarifa yake Gutteres ametoa wito wa kutafutwa njia ya amani iloi kutanzua mzozo huo.

Huko Kiyv rais Volodymyr Zelensky ametoa wito kwa mataifa ya dunia kulaani kitendo hicho na kuiwekea vikwazo Rashia akisema anatafakari pia juu ya kuvunja uhusiano na Moscow.

“Nimepokea ombi kutoka kwa wizara ya mambo ya nje kutathmini suala la kuvunja uhuisano kati ya Ukraine na Shirikisho la Rashia. Nitalitahmini suala hilo na kulishughulikia mara tu baada ya kumaliza mkutano huu na nyinyi waandishi habari,” alisema Zelensky

Kremlin nako, kupitia msemaji wake Dmitry Peskov imesema kwamba ina matumaini kua Rashia kutyatambua majimbo mawili ya Ukriane yanayotaka kujitenga ili kuwa huru kutasaidia kurudisha utulivu na kwamba Moscow inagli iko tayari kwa mazungumzo ya kidiplomasia na Marekani na mataifa mengine.

XS
SM
MD
LG