Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 28, 2024 Local time: 07:30

White House inaweka vikwazo kwa maeneo ya mashariki mwa Ukraine


Wanaharakati wanaounga mkono Russia katika mtaa wa Donetsk huko Ukraine
Wanaharakati wanaounga mkono Russia katika mtaa wa Donetsk huko Ukraine

White House ilisema Jumatatu itaweka vikwazo kwa maeneo yanayozungumza ki-Russia ya Donetsk na Luhansk huko mashariki mwa Ukraine, saa chache baada ya Rais wa Russia Vladmir Putin kuyatambua kuwa mataifa huru.

Matamshi hayo ya Putin yanaongeza hofu kwa nchi za magharibi kwmaba Putin yuko mbioni kuivamia Ukraine. Tulitarajia hatua kama hii kutoka Russia na tuko tayari kujibu mara moja, msemaji wa White House Jen Psaki alisema Jumatatu.

Rais Biden hivi karibuni atatoa amri ya kiutendaji ambayo itadhibiti uwekezaji mpya, biashara, na ufadhili wa watu wa Marekani kwenda, kutoka au katika yale yaliyokuwa yanaitwa maeneo ya Jamhuri ya watu wa Donetsk (DNR) na Jamhuri ya watu wa Luhansk (LNR) ya Ukraine. Amri hii ya kiutendaji pia itatoa mamlaka ya kuweka vikwazo kwa mtu yeyote aliyedhamiria kufanya kazi katika maeneo hayo ya Ukraine.

XS
SM
MD
LG