Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 00:31

Russia yadaiwa kombora lake limetua karibu na kinu cha nyuklia Ukraine


Shambulizi la kombora lililofanywa na jeshi la Russia karibu na kinu cha nyuklia cha Pivdennoukrainsk Sept 19, 2022.
Shambulizi la kombora lililofanywa na jeshi la Russia karibu na kinu cha nyuklia cha Pivdennoukrainsk Sept 19, 2022.

Kampuni inayoendesha nishati ya nyuklia Ukraine ilisema Jumatatu kuwa kombora la Russia limepiga karibu na kinu cha nishati ya nyuklia huko kusini mwa Ukraine.

Kampuni hiyo Energoatom ilisema katika taarifa yake kwamba kombora hilo lilitua mita 300 kutoka katika Kinu cha Nishati ya Nyuklia cha Pivdennoukrainsk lakini haijaharibu machine zake.

Shambulizi hilo limeharibu majengo yaliyoko karibu, Energoatom ilisema.

“Russia inahatarisha usalama wa dunia nzima,” Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema katika ujumbe wa Telegram akijibu shambulizi hilo la kombora. “Ni lazima tusitishe hatari hii kabla haijakuwa tumechelewa.”

Mtambo wa Pivdennoukrainsk ni kinu kikubwa kabisa cha pili cha nishati ya nyuklia cha Ukraine, Kinu cha Nishati ya Nyuklia cha Zaporizhzhia, tayari kimefungwa tangu mapema Septemba baada ya mashambulizi kuendelea ambapo Russia na Ukraine zinalaumiana kuhusika.

Zelenskyy alisema Jumapili hakutakuwa na kulegalega katika juhudi za jeshi la nchi yake kulichukua eneo hilo kutoka katika uvamizi wa majeshi ya Russia.

Kauli ya Zelenskyy – aliyoitoa wakati wa hotuba zake za usiku kila siku – zinafuatia majeshi ya Ukraine kupata mafanikio katika mkoa wa Kharkiv huko kaskazini masharik mwa Ukraine wakati wakijibu mashambulizi dhidi ya Russia mwezi huu.

“Pengine hivi sasa inaelekea kwa baadhi yenu kuwa baada ya ushindi kadhaa tuna aina fulani ya kulegeza Kamba,” Zelenskyy alisema. “Lakini alisema hakuna kulegeza kamba. Haya ni matayarisho kwa ajili ya hatua kadhaa zijazo… kwa sababu Ukraine lazima iwe huru – nchi nzima.”

Rais wa Marekani Joe Biden alisema katika mahojiano na kituo cha televisheni cha CBS katika kipindi cha “60 Minutes” kuwa Ukraine, kupitia msaada wa Umoja wa Mataifa na washirika wake, pia “ushujaa wa ajabu na kuazimia kwa watu wa Ukraine” hawajaemea katika vita hii.

Biden alisema kushinda vita maana yake ni “kuiondoa Russia kutoka Ukraine” na kutambua haki ya Ukraine kujitawala.

Alipoulizwa kuhusu msaada wa kijeshi na kibinadamu ambao Marekani imeahidi kwa Ukraine, Biden alisema Marekani itaendelea kuisaidia Ukraine “kwa muda wote utakaohitajika.”

XS
SM
MD
LG