Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 21:06

Russia yadai meli yake ya mafuta karibu na Cremia imeshambuliwa na Ukraine


Meli ya Russia inayodaiwa kushambuliwa na ndege isiyo na rubani ya Ukraine
Meli ya Russia inayodaiwa kushambuliwa na ndege isiyo na rubani ya Ukraine

Maafisa wa ulinzi wa bahari wa Russia walithibitisha Jumamosi kwamba shambulio la ndege isiyo na rubani ya Ukraine iliharibu meli ya Russia, iliyokuwa na idhini ya kuwepo, karibu na daraja la kimkakati linalounganisha Crimea na Russia bara.

Shambulizi hilo lilisababisha kusimamishwa kwa usafirishaji wa bidhaa na huduma za feri.

Kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya Russia, meli hiyo ya mafuta ilikuwa ikikaribia Mlango-Bahari wa Kerch, unaounganisha Bahari ya Black Sea na ile ya Azov, ilipogongwa na ndege zisizo na rubani za Ukraine.

Meli hiyo ya kubeba bidhaa za kemikali iliidhinishwa na Marekani mnamo mwaka wa 2019 ili kusaidia kusafirisha mafuta ya ndege kwa vikosi vya Russia nchini Syria.

Habari za shambulio hilo zinafuatia jingine lililoharibu vibaya meli ya kivita ya Russia katika kituo cha wanamaji cha Black Sea.

Vikosi vya Ukraine vimesema vinavunja safu ya ulinzi ya kusini mwa Russia, na kuhamia "ya kati," Naibu Waziri wa Ulinzi Hanna Maliar aliripoti Ijumaa.

Usiku wa kuamkia Jumamosi meli ya kivita ya Russia iliharibiwa vibaya kufuatia shambulizi la ndege isiyo na rubani ya Ukraine katika kambi ya jeshi la wanamaji ya Novo-ro-ssi-ysky, katika bahari ya Black Sea.

Forum

XS
SM
MD
LG