Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 17:05

Russia yadai kuuteka mji wa Mariupol, yaendeleza mashambulizi mashariki


Rais wa Russia Vladimir Putin (kulia) na Waziri wake wa Ulinzi Sergei Shoigu
Rais wa Russia Vladimir Putin (kulia) na Waziri wake wa Ulinzi Sergei Shoigu

Waziri wa Ulinzi wa Russia Sergei Shoigu amemwambia Rais Vladimir Putin kuwa vyote viwili kiwanda cha chuma cha Azovstal na mji wenyewe “umekombolewa kikamilifu.” Kulingana na taarifa ya Wizara ya Ulinzi ya Russia.

Hakuna uthibitisho wa papohapo kutoka Ukraine kwamba mji wa Mariupol ulikuwa chini ya udhibiti kamili wa Russia.

Mji huo wa bandari ni sehemu iliyozingirwa na umwagaji damu, huku majeshi ya Russia waliushambulia kwa mabomu takriban kwa miezi mitatu. Sehemu kubwa ya Mariupol imegeuka kuwa ni kifusi, na zaidi ya raia 20,000 wanahofiwa wamefariki.

Wapiganaji wa Ukraine ambao wanajificha katika kiwanda hicho cha chuma cha mji huo walikuwa wanakabiliana na mapigano makali yaliokuwa yanaelekezwa na majeshi ya Russia kwa wiki kadhaa. Mapema wiki hii, hata hivyo, maafisa wa Ukraine waliwaamuru wapiganaji kusalimu amri ili kuokoa maisha yao.

Operesheni ya kuwaondoa wapiganaji wa mwisho kutoka katika kiwanda cha chuma cha
Azovstal, ambao idadi yao haijulikani, ilifuatiwa na wanajeshi wa Ukraine takriban 2,000 kujisalimisha katika siku za hivi karibuni, kulingana na Waziri wa ulinzi wa Russia.

Kamanda wa Kikosi cha Azov cha Ukraine, waliokuwa vinara wa kulinda kiwanda hicho, walisema juhudi za kuondoa miili ya waliokufa kutokana na mapigano hayo ilikuwa inaendelea.

XS
SM
MD
LG