Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 04:40

Biden akutana na viongozi wa Finland, Sweden kujadili upanuzi wa NATO


UKRAINE-CRISIS/NATO-BIDEN
UKRAINE-CRISIS/NATO-BIDEN

Rais wa Marekani Joe Biden amekutana na viongozi wa Sweden na Finland Alhamisi baada ya nchi hizo kuweka kando msimamo wao wa muda mrefu wa kutoegemea upande  wowote  na kutaka kujiunga na  muungano wa NATO kujibu uvamizi wa Russia nchini Ukraine. 

Saa chache kabla ya safari yake ya kwanza katika bara la Asia kama Rais, Biden alikutana na Waziri Mkuu wa Sweden Magdalena Andersson na Rais wa Finland Sauli Niinisto katika ikulu kujadiliana kuhusu maombi yao kujiunga na NATO.

“ Hili ni tukio la kihistoria, mabadiliko katika usalama wa Ulaya. Mataifa mawili yenye utamaduni wa kuegemea upande mmoja watajiunga katika ushirikiano wenye nguvu wa usalama duniani, amesema hayo mshauri wa usalama wa White House , Jake Sullivan.”

Biden ameweka kipaumbele kikubwa cha Ulaya kuungana dhidi ya uvamizi wa Russia huko Ukraine.

Uturuki imehoji kuhusu kuziweka Finland na Sweden katika Umoja huo, ikitaka Sweden kuacha kuwaunga mkono wanamgambo wa kikurdi ambao inawaona kama kundi la kigaidi na wote kuondoa marufuku zao katika baadhi ya mauzo ya silaha kwa Uturuki.

XS
SM
MD
LG