Baraza la seneti la Marekani lilikamilisha hatua ya bunge Alhamis kuhusu msaada mpya wa dola bilioni 40 kwa Ukraine umeidhinishwa kwa idadi kubwa na kuwasilisha hatua hiyo kwa Rais Joe Biden kwa ajili ya kutia saini.
Msaada huo una azma ya kuisaidia Ukraine katika muda wa miezi mitano ijayo kupambana na uvamizi unaoendelea wa Russia. Unajumuisha fedha kwa ajili ya vifaa vya kijeshi, mafunzo na silaha, pamoja na mabilioni ya dola kwa misaada ya kibinadamu, ikiwa ni pamoja na fedha za kusaidia kukabiliana na uhaba wa chakula duniani uliosababishwa na mgogoro wa miezi mitatu.
Msaada huo unaongezea akiba ya vifaa vya Marekani vilivyotumwa awali nchini Ukraine na kutoa msaada wa fedha kuzisaidia nchi nyingine ambazo zinaisaidia serikali ya Kyiv.
Kura za seneti ambazo ni 86 dhidi ya 11 zilikuwa juu ya kura zilizopigwa kuunga mkono sheria katika baraza la wawakilishi wiki iliyopita ikionyesha uungaji mkono Marekani kwa Ukraine wakati ambapo bunge ambalo mara kwa mara limegawanyika katika masuala makuu yanayotokea kila siku.