Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 04:34

Wapiganaji 700 wa Ukraine wajisalimisha


Wanajeshi wa Russia wakitekeleza mashambulizi karibu na kiwanda cha chuma cha Azovstal, Mariupol, Ukraine May 5, 2022. PICHA: REUTERS
Wanajeshi wa Russia wakitekeleza mashambulizi karibu na kiwanda cha chuma cha Azovstal, Mariupol, Ukraine May 5, 2022. PICHA: REUTERS

Russia imesema kwamba karibu wapiganaji 700 wa Ukraine waliokuwa katika kiwanda cha chuma cha Mariupol wamejisalimisha katika saa 24 zilizopita.

Viongozi wa wapiganaji hao wanaripotiwa kuwa bado ndani ya kiwanda hicho.

Wizara ya ulinzi ya Russia imesema kwamba kwa jumla, wapiganaji 959 waliokuwa katika kiwanda hicho cha mjini Azavstal, wamejisalimisha kwa jeshi la Russia.

Kiongozi wa kundi la wapiganaji linaloungwa mkono na Russia, na linalodhibithi sehemu hiyo Denis Pushilin, amesema kwamba kwamba makamanda wa wapiganaji hao waliokuwa ndani ya kiwanda hawajajisalimisha.

Endapo wapiganaji hao wote watajisalimisha, hatua yao itafikisha mwisho wa mapigano ya miezi mitatu ambayo yameharibu kabisa mji wa Mariupol wenye wakaazi 400,000, na uliokuwa na maendeleo makubwa lakini kwa sasa umeharibiwa kabisa kutokana na vita.

Ukraine inasema kwamba maelfu ya raia wamekufa kutokana na mashambulizi ya Rusia, na wengi wamezikwa katika makaburi ya pamoja.

Russia imesema kwamba zaidi ya wapiganaji 50 wa Ukriane wanapokea matibabu hospitalini na wengine wanazuiliwa katika gereza jipya katika miji inayoshikiliwa na wapiganaji wanaoungwa mkono na Russia.

XS
SM
MD
LG