Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 26, 2025 Local time: 09:51

Ripoti ya RSF: Shambulizi la waandishi wa habari Lebanon lilikusudiwa na Israel


Mwanamke akishikilia picha ya mwandishi Issam Abdallah, aliyeuawa Oktoba 13 katika kijiji Alma al-Shaab kusini mwa Lebanon, wakati wa maandamano ya kupinga mauaji hayo huko Beirut, Oktoba. 15, 2023.
Mwanamke akishikilia picha ya mwandishi Issam Abdallah, aliyeuawa Oktoba 13 katika kijiji Alma al-Shaab kusini mwa Lebanon, wakati wa maandamano ya kupinga mauaji hayo huko Beirut, Oktoba. 15, 2023.

Mwandishi anayepiga picha za video Issam Abdallah alifariki na waandishi wengine sita kujeruhiwa – wawili kati yao ni waandishi wa AFP, mmoja alijeruhiwa vibaya sana – katika mashambulizi kwenye kiji cha Alma al-Shaab kusini mwa Lebanon Oktoba 13.

“Ugunduzi wa awali unaonyesha kuwa waandishi hao walikuwa siyo waathirika wakuu wa shambulizi hilo la kombora,” kundi linalofuatilia vyombo vya habari la Reporters Without Borders (RSF).

“Moja ya magari yao, ambayo yalikuwa na nembo ya ‘press’, yalilengwa, na pia ilikuwa bayana kuwa kundi hilo lilikuwa pembeni yao na waandishi wa habari,” RSF ilisema.

Waandishi hao wanaamini kuwa walishambuliwa kutokea upande wa mpaka wa Israeli.

Ugunduzi wa awali wa RSF haukuyalaumu moja kwa moja majeshi ya Israeli, lakini ilisema kuwa kulingana na tathmini ya kombora, mashambulizi yalitokea upande wa mashariki, ikiwa ni upande wa mpaka wa Isreali.

Uchunguzi wa RSF ulibaini kuwa mashambulizi mawili katika sekunde 37 na 38 yakipishana yalipiga eneo ambako kikundi cha waandishi saba walikuwepo hapo kwa zaidi ya saa moja.

Shambulizi la kwanza lilimuua Abdallah, na la pili, ambalo lilikuwa lenye nguvu zaidi, liliilipua gari iliyokuwa inatumiwa na Al-Jazeera, na kuwajeruhi waandishi kadhaa. RSF ilisema inaendelea na uchunguzi wake.

Mamlaka nchini Lebanon zimeishutumu Israel kuhusika na mashambulizi hayo.

Jeshi la Israeli lilisema lilikuwa linataka kufahamu mazingira yaliyopelekea shambulizi hilo lililouwa.

AFP inafanya uchunguzi wake binafsi kuhusiana na shambulizi hilo na limeitaka Israel na Lebanon kufanya uchunguzi wa kina.

Reuters iliitaka pia Israel kufanya uchunguzi wa haraka na kamili.

Mpaka kati ya Israeli na Lebanon umekumbwa na ghasia tangu kikundi cha kikundic ha wanamgambo wa Palestina, Hamas kilipouwa watu 1,400, wengi wao wakiwa ni raia, katika shambulizi walilolifanya Oktoba 7 dhidi ya Israel, na kuzusha ulipizaji kisasi wa mashambulizi ya mabomu huko Gaza ambayo yameuwa zaidi wa watu 8,000, wengi wao raia, kulingana na wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas huko Gaza.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP.

Forum

XS
SM
MD
LG