Jeshi la anga la Israel limesema limeshambulia malengo zaidi ya 600 ya Hamas huko Gaza katika kipindi cha saa 24. Israel imesema pia imeshambulia maeneo nchini Syria na Lebanon.
Mashambulizi ambayo jeshi la Israel lilisema Jumatatu ni kujibu mashambulizi yaliyofanywa kutoka nchi zote mbili. Shirika la Save the Children limesema katika taarifa yake kwamba idadi ya watoto wanaoripotiwa kuuawa Gaza katika kipindi cha wiki tatu “kimevuka idadi ya kila mwaka ya watoto wanaouawa kote katika maeneo yenye mizozo duniani tangu mwaka 2019”.
Zaidi ya watoto 3,000 wameuawa katika mzozo kati ya Israel na Gaza.
Israel imechapisha picha za vifaru vyake katika pwani ya magharibi ya Palestina saa 48 baada ya kuamuru kupanua uvamizi wake wa ardhini kote katika maeneo mashariki mwa mpaka. Hamas imesema imeshambulia vifaru vya Israel kaskazini mwa Gaza kwa makombora na kukejeli taarifa kwamba wanajeshi wa Israel wameingia Gaza. Hakuna ripoti inayoweza kuthibitishwa na vyanzo uhuru.
Forum