Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 16:16

Marekani yaihimiza Israel kuwalinda raia, kuongeza msaada kwa Gaza


Moshi mkubwa watanda juu ya Gaza, kufuatia mashambulio ya mabomu ya Israel
Moshi mkubwa watanda juu ya Gaza, kufuatia mashambulio ya mabomu ya Israel

Marekani inaishinikiza Israel kuchukua tahadhari katika kuwalinda raia wa Gaza na kutaka kuongezwa mara moja msaada wa dharura, wakati kukiwa na kilio kutokana na idadi kubwa ya vifo na wanaojeruhiwa kutokana na wiki tatu za kudondoshwa mabomu.

Rais Joe Biden wa Marekani alizungumza kwa njia ya simu na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, na kuthibitisha tena haki ya Israel kulinda raia wake, lakini kwa kuambatana na sheria za kimataifa kuhusu kulinda raia.

Viongozi hao wawili walizungumza pia juu ya juhudi za kuwalinda karibu mateka 200 walochukuliwa na kundi la wanamgambo la Hamas tangu oktoba 7, kufuatia shambulio lililosababisha vifo vya watu 1, 400 ndani ya Israel.

Rais Joe Biden akihutubia taifa suala la Israel na Palestina kutokea ofisini kwake, Oval Office.
Rais Joe Biden akihutubia taifa suala la Israel na Palestina kutokea ofisini kwake, Oval Office.

Taarifa ya White House inaeleza kwamba Biden, "alisisitiza juu ya umuhimu wa kuongeza kwa haraka na kwa kiwango kikubwa msaada wa dharura ili kukidhi mahitaji ya wakazi wa Gaza."

Biden anakabiliwa na shinikizo ndani ya chama chake cha Demokratik kumtaka atowe wito wa kusitishwa mapigano.

"Kama muungaji mkono mkubwa wa kijeshi wa Israel, Marekani inawajibika kwa sehemu fulani kwa mambo yanayotokea Gaza," alisema Pramila Jaypal, mbunge Mdemokrat, alipozungumza na kipindi cha "Meet The Press," cha NBC.

Biden alizungumza pia Jumapili na Rais Abdel Fatah al-Sisis na kumshukuru kiongozi huyo wa Misri kwa jukumu lake la kuwasilisha msaada wa dharura huko Gaza.

Walikubaliana kufanya kazi pamoja kuweka masharti ya kuwepo na amani ya kudumu Mashariki ya Kati pamoja na kuundwa kwa taifa la Wapalestina.

Israel yaongeza mashambulizi Gaza

Picha iliyochukuliwa kusini mwa Israel kwenye mpaka na Ukanda wa Gaza ikionesha vifaru vya Israel na buldoza zikivuka mpaka kuingia Gaza, Oktoba 29, 2023.
Picha iliyochukuliwa kusini mwa Israel kwenye mpaka na Ukanda wa Gaza ikionesha vifaru vya Israel na buldoza zikivuka mpaka kuingia Gaza, Oktoba 29, 2023.

Maafisa wa jeshi la Israel walisema Jumapili kwamba mashambulio yake ya nchi kavu na anga yameongezwa dhidi ya vituo vya Hamas kwenye Ukanda wa Gaza. Nao wapiganaji wa Hamas wameripoti kuwepo na mapigano makali kaskazini mgharibi ya Gaza.

Israel ilichapisha picha za vifaru vyake ndani upande wa pwani ya magharibi ya Ukanda huo saa 48 baada ya kutolewa amri ya kuanza mashambulio ya nchi kavu kupitia mpaka wa mashariki.

Wapiganaji wa Hamas nao wanasema wameshambulia vifaru vya Israel kwa makombora na kukanusha ripoti kwamba wanajeshi ya Israel wamesonga ndani kabisa ya Gaza.

Hakuna ripoti kati ya hizi zilizoweza kuthibitishwa na njia huru.

Forum

XS
SM
MD
LG