Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 20:00

Israel yaomba wakazi wa Gaza waelekee kusini wakati ikiongeza mashambulizi ya ardhini


Moshi ukipaa angani kufuatia mashambulizi ya Israel kwenye eneo la mpaka na Ukanda wa Gaza Oktoba 27, 2023 (Picha na Menahem KAHANA / AFP)
Moshi ukipaa angani kufuatia mashambulizi ya Israel kwenye eneo la mpaka na Ukanda wa Gaza Oktoba 27, 2023 (Picha na Menahem KAHANA / AFP)

Siku mbili tu baada ya Israel kutuma wanajeshi wake Ukanda wa  Gaza, jeshi la Israel kwa mara nyingine linawasihi wakazi waelekee upande wa kusini, huku mashambulizi ya anga yakiendelea upande wa kaskazini.

Hiyo ni kama sehemu ya hatua pana za kivita dhidi ya wanamgambo wa Hamas. Idara ya Ulinizi ya Israel IDF imesema Jumapili kwamba ndege zake za kivita zimepiga malengo 450 ya Hamas huko Gaza katika saa 24 zilizopita, ikiwa pamoja na kufanya mashambulizi a karibu na hospitali ya Shifa, ambayo ni moja ya hospitali kubwa sana huko Gaza, ikiwa imejaa wagonjwa, pamoja na kuwa hifadhi kwa wale wanaotoroka mapigano.

Msemaji wa IDF Daniel Hagari kupitia video iliyowekwa kwenye mtandao wa X uliokuwa zamani ukijulikana kama Twitter mapema leo amesema, “magaidi wa Hamas wanafanyia operesheni zao kwenye majengo ya raia kwa kuwa wanafahamu kwamba IDF inatofautisha kati ya magaidi na raia.” Ameongeza kusema kwamba jeshi lake linapanua mashambulizi, na kwa hivyo kuomba raia waondoke karibu na ngome za Hamas.

Forum

XS
SM
MD
LG