Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 10:51

Rikodi Mpya ya Marathon : Kipchoge akamilisha marathon chini ya masaa mawili


Eliud Kipchoge wa Kenya akifurahia ushindi wake baada ya kuvunja rikodi ya mbio za marathon za masaa mawili Oct. 12, 2019, in Vienna.
Eliud Kipchoge wa Kenya akifurahia ushindi wake baada ya kuvunja rikodi ya mbio za marathon za masaa mawili Oct. 12, 2019, in Vienna.

Mbio maalum alizoshiriki Eliud Kipchoge huko Vienna, Austria zimemfanya kuwa mwanariadha wa kwanza duniani kuvunja rikodi ya mbio za marathon kwa kukimbia kilomita 42 chini ya saa mawili, Shirika la habari la Uingereza Reuters limeripoti.

Kipchoge, mwenye umri wa miaka 34, ambaye ni raia wa Kenya alikimbia muda wa kilomita 42.2 katika saa moja dakika 59 na sekunde 40 katika mbio hizo zilizofanyika Ineos Challenge mjini Vienna nchini Austria siku ya Jumamosi.

Kwa hivyo ameweza kupunguza sekunde ishirini katika mbio hizo na kuweza kuvunja rikodi iliyowekwa miaka 65 iliyopita.

Mwanariadha huyo mashuhuri duniani amelinganisha mbio hizo na mtu wa kwanza kwenda mwezini, kabla ya kuanza kukimbia alisema kwamba ameweka historia sawa na raia wa Uingereza Sir Roger Bannister alivyofanya wakati alipokuwa mtu wa kwanza kukimbia maili moja chini ya dakika nne mwaka 1954.

''Nahisi vyema, baada ya Roger Bannister kuweka historia ilinichukua miaka 65. Nimejaribu lakini nimevunja,” alisema raia huyo wa Kenya.

''Hii inaonyesha uzuri wa michezo. Nataka kuufanya mchezo huu kuwa safi na wa kufurahisha. Pamoja tunapokimbia tunafanya ulimwengu kuwa mzuri wa kuishi,” alisema Kipchoge.

Bingwa huyo wa Olimpiki alikuwa ameikosa rekodi hiyo kwa sekunde 25 katika jaribio lake la hapo awali 2017.

Hata hivyo mafanikio hayo hayataingia katikarikodi mpya ya dunia katika mbio hizo kwani hilo halikuwa shindano. Kundi la wanariadha lilitumika siyo kwa mashindano bali kusaidia kusukuma kasi ya mbio hizo.

Wakati ilipofahamika kuwa anakaribia kuvunja rikodi hiyo ya dunia, wanariadha walioambatana naye wakati wa mbio hizo ili kudhibiti kasi ya mbio hizo walirudi nyuma na kumwacha bingwa huyo kutimka hadi katika utepe huku akishangiliwa na mashabiki wengi katika mji mkuu wa Austria.

XS
SM
MD
LG