Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 10:12

Wanariadha wa Afrika Mashariki kujaribu kuvunja rekodi ya marathon


Marathon ya Afrika Mashariki
Marathon ya Afrika Mashariki

Jumamosi wanariadha watatu mashuhuri kutoka Afrika Mashariki watajitahidi kufanya kitu ambacho hakijawahi kufanyika: kumaliza mbio za Marathon kwa muda usiozidi masaa mawili.

Eliud Kipchoge wa Kenya, Lelisa Desisa wa Ethiopia pamoja na Zersenay Tadese kutoka Eritrea watakimbia kwenye uwanja uliofunikwa wenye urefu wa kilomita 2.4 mjini Monza, Italy, ambapo wataalamu wanasema kuwa unafaa kwa mbio hizo.

Mwandishi wa Idhaa ya Kiswahili VOA ameripoti kuwa mbio hizo zimefadhiliwa na kampuni ya Nike ambayo hivi karibuni ilizindua mradi maarufu kama “moonshot” wenye nia ya kuvunja rekodi ya muda wa saa mbili kwenye mbio za marathon.

Anaeshikilia rekodi ya dunia kwa sasa ni Dennis Kimetto kutoka Kenya alishinda kwenye mbio za Berlin Marathon 2014.

Wesly Korir kutoka Kenya ambaye ni mshindi wa Boston Marathon 2012 amezungumza na Idhaa ya Kiswahili VOA na kusema kuwa anaamini kuwa rekodi ya saa mbili ni jambo linalowezekana.

Korir anasema kuwa kwa mwanariadha kujaribu kukimbia kwa kipindi cha chini ya saa mbili ni swala linalovuta uwezo wa binadamu hadi mwisho. Ili kuvunja rekodi, wanariadha wanahitaji kuongeza kasi ya sekunde 7 kwa kila maili.

please wait

No media source currently available

0:00 0:04:07 0:00

Imetayarishwa na Mwandishi wetu Harrison Kamau, Washington DC

XS
SM
MD
LG