Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:15

Warepublikan wasukuma muswada wa afya Baraza la Seneti


Rais Donald Trump na Makamu wa Rais Mike Pence wakisherekea ushindi wa muswada wa Afya
Rais Donald Trump na Makamu wa Rais Mike Pence wakisherekea ushindi wa muswada wa Afya

Rais Donald Trump na Warepublikan katika Bunge walimaliza mapambano makali katika kupitisha mswada wa Afya kwa kusheherekea ushindi ikulu ya White House Alhamisi.

Hii ni hatua ya kwanza ya Wabunge hao kuonja mafanikio ya utawala katika ushindi wa kwanza mkubwa kupitishwa na Bunge .

Ushindi umeipa ikulu ya White House na Bunge la Warepublikan zoezi muhimu katika kufanya kazi pamoja wiki kadhaa baada ya kushindwa katika jaribio la kwanza kuibadilisha Sheria ya Affordable Care ambayo ni maarufu kwa jina la Obamacare.

Trump na Makamu wa Rais Mike Pence waliongeza juhudi ya kufanya mazungumzo kwa raundi ya pili, wakiandaa muswada uliopitishwa kwa kura zenye kujitosheleza ili kuweza kupelekwa kwa ajili ya kujadiliwa na Baraza la Seneti.

Ikulu ya White House hivi sasa inakabiliwa na kazi ngumu ya kuweza kushawishi muswada wa Afya kupitishwa kwa kura ambazo ni za chache zaidi katika Seneti. Akiwa pamoja na Wabunge wa Republikan wenye kujawa na furaha waliomzunguka hapo white House kwenye bustani ya Rose Garden, Trump aliahidi ushindi.

“Itakuwa ni ushindi wa ajabu wakati muswada huu ukipitishwa kwenye Baraza la Seneti,”

XS
SM
MD
LG