Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:11

Kipchoge aibuka kidedea mara ya nne mashindano ya London Marathon


 Eliud Kipchoge
Eliud Kipchoge

Mwanariadha mashuhuri na mshindi wa mbio za Olympiki duniani Eliud Kipchoge ameshinda tena mbio za London Marathon 2019, kwa mara ya nne mfululizo.

Kipchoge raia wa Kenya, 34, ambaye alifanikiwa kuvunja rekodi ya dunia ya mbio hizo mjini Berlin 2018, alikamilisha mbio za Jumapili kwa muda wa saa mbili dakika mbili na sekunde thelathini na nane (2: 02: 38.) zilizofanyika katika mji mkuu wa Uingereza.

Vyanzo vya habari vimeeleza kuwa Kipchoge aliwabwaga wanariadha Mosinet Geremew na Mule Wasihun raia wa Ethiopia ambao waliweza kumaliza mbio hizo katika nafasi ya pili na ya tatu.

Hata hivyo Kipchoge ambaye alishinda mwaka 2015, 2016 and 2018 mbio hizo za Marathon, hakuweza kuipiku rekodi yake ya Dunia ya sekunde 59 ambayo ilikuwa 2:01:39 aliyokuwa ameiweka katika shindano la mwaka uliopita.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Uingereza, BBC, Mo Farah, raia wa Uingereza alichukuwa nafasi ya tano baada ya kumaliza dakika 3 na sekunde moja nyuma ya Kipchoge, huku Callum Hawkins kutoka Uingereza akimaliza katika nafasi ya 10.

Pia imesema kuwa Brigid Kosgei, 25, raia wa Kenya alishinda mbio hizo upande wa wanawake na kuwa mwanamke wa kwanza wa umri mdogo kushinda London marathon.

Mwengine ni Kosgei aliyeweza kumshinda bingwa mtetezi Vivian Cheruiyot kwa kutumia mda wa saa 2:18:20 kushinda mbio hizo kwa mara ya kwanza.

Imeongeza kuwa Mkenya Vivian Cheruiyot alichukua nafasi ya pili huku Roza Dereje wa Ethiopia akimaliza wa tatu. Muingereza Charlotte Purdue alimaliza nafasi ya 10.

XS
SM
MD
LG