Zambia ilikuwa na deni la bilioni 18.6 wakati iliposhindwa kulipa mwaka 2020, na kufikia makubaliano kimsingi katika mwezi Oktoba na wakopeshaji wa kigeni.
Hichilema amesema kuwa takriban asilimia 98 ya wakopeshaji rasmi kwa sasa wamesaini waraka wa maelewano kurekebisha deni la Zambia ambalo linakadiriwa kufikia dola bilioni 32.8 ilipofikia mwaka 2022.
“Hiyo ni hatua kubwa” aliuambia mkutano wa waandishi wa habari katika mji mkuu Lusaka.
Lakini mazungunzo binafsi wa wakopeshaji yamekwama, amesema.
“Bado tunashauriana” alisema Hichilema.
Mzozo huo juu ya “ulinganifu wa huduma” chini ya kanuni ya kurekebisha muundo wa madeni kwa nchi masikini sana uliokubaliwa na kundi ka G20, alisema.
Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la AFP
Forum