Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 30, 2024 Local time: 20:02

Wachimbaji haramu wa madini 7 wathibitishwa kufariki na wengine zaidi ya 20 hawajulikani waliko


Wafanyakazi wa migodini wanaonekana wakati wa kazi ya uokoaji huko Chingola, karibu kilomita 400 kaskazini mwa mji mkuu wa Lusaka, Zambia, Jumamosi, Desemba 2, 2023.
Wafanyakazi wa migodini wanaonekana wakati wa kazi ya uokoaji huko Chingola, karibu kilomita 400 kaskazini mwa mji mkuu wa Lusaka, Zambia, Jumamosi, Desemba 2, 2023.

Washukiwa saba wachimba haramu wa madini walithibitishwa kufariki dunia na wengine zaidi ya 20 hawajulikani waliko na kudhaniwa wamekufa baada ya mvua kubwa kusababisha maporomoko ya ardhi.

Washukiwa saba wachimba haramu wa madini walithibitishwa kufariki dunia na wengine zaidi ya 20 hawajulikani waliko na kudhaniwa wamekufa baada ya mvua kubwa kusababisha maporomoko ya ardhi yaliyowafukia ndani ya mahandaki waliyokuwa wakichimba kwenye mgodi wa shaba nchini Zambia, polisi na mamlaka nchini humo walisema Jumamosi.

Polisi walitoa majina au baadhi ya majina ya waathirika saba waliothibitishwa na kusema wachimba migodi wote kwenye mahandaki wanashukiwa kufariki. Polisi hawakusema ni wachimbaji wangapi kwa jumla walikuwa kwenye mahandaki lakini Mkuu wa Wilaya ya Chingola Raphael Chumupi aliambia Associated Press kwamba kulikuwa na takriban watu 36.

Maafisa wa serikali walisema kuwa zaidi ya wachimba migodi 30 walikwama kwenye mahandaki lakini hawakuweza kutaja idadi kamili.

Forum

XS
SM
MD
LG