Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 22:23

Spika wa Bunge la Kenya apiga marufuku mavazi yasiyofaa


Picha ya wabunge wa Kenya wakiwa ndani ya Bunge
Picha ya wabunge wa Kenya wakiwa ndani ya Bunge

Spika wa bunge la Kenya amepiga marufuku kile alichokieleza kuwa mavazi yasiyofaa yanayovaliwa na wabunge, hata kupiga marufuku vazi la kitamaduni la kiafrika na suti zinazopendwa na Rais William Ruto.

Moses Wentan’ugula aliwambia wabunge Jumanne kuwa lazima waheshimu sheria za mavazi za bunge, akikemea “mitindo inayoibuka ambayo sasa inatishia kanuni za mavazi za bunge.”

Amesema kile kinachoitwa suti aliyokuwa akipenda kuvaa hayati rais wa Zambia Kenneth Kaunda, limepigwa marufuku pia, pamoja na mavazi ya kitamaduni yasiyofaa.

Ruto huvaa mara nyingi suti za kawaida, lakini vazi la Kaunda sasa ndilo vazi lake analolipenda, na alilivaa wakati wa ziara ya Mfalme Charles wa tatu mapema mwezi huu.

Kulingana na kanuni za Spika, “vazi linalofaa kwa wanaume ni kanzu, kola, tai, shati la mikono mirefu, suruali ndefu, soksi na viatu.”

Kwa wanawake, sketi, na nguo lazima iwe chini ya goti na juu ya mikono, isiyokuwa na mikono ni marufuku.

Forum

XS
SM
MD
LG