Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 09:41

Rais Ruto: Kenya haitashindwa kulipa madeni yake

Rais wa Kenya William Ruto
Rais wa Kenya William Ruto

Rais wa Kenya William Ruto amesema serikali yake itaimarisha ukusanyaji wa ushuru na kupunguza ukopaji huku akiahidi nchi hiyo ya Afrika Mashariki haitashindwa kulipa madeni yake.

Rais wa Kenya William Ruto amesema serikali yake itaimarisha ukusanyaji wa ushuru na kupunguza ukopaji huku akiahidi nchi hiyo ya Afrika Mashariki haitashindwa kulipa madeni yake.

Katika mahojiano kuhusu masuala mbalimbali na vyombo vya habari vya Kenya jumatano, rais Ruto amesema Kenya haitoshindwa kulipa deni lake.

Kenya imekabiliwa na deni wakati wa ukarabati wa miundombinu ikiwemo reli na barabara chini ya rais wa zamani Uhuru Kenyatta.

Mwaka 2022 shirika la Fitch linalofuatilia madeni, lilionya kuwa viwango vya madeni na viwango vya riba vya kimataifa kwa serikali vinaongeza hatari ya kushushwa kiwango cha kukopa kama ilivyo kwa takriban nchi 10 za Afrika.

Kenya ikitajwa kuwa moja miongoni mwa nchi zilizo katika hatari kubwa.

Tangu serikali ya Ruto iliposhika hatamu za uongozi mwezi Septemba iliahidi kupambana na ukopaji wa gharama kubwa za kibiashara kwa ajili ya vyanzo vya bei nafuu kama Benki ya Dunia.

Akizungumzia baadhi ya mipango ya serikali yake ambayo tayari inafanyakazi katika kuwasaidia vijana Rais Ruto alisema fuko la Hutsler ni moja wapo ya mipango inayofanya kazi vizuri kwa hivi sasa.

FILE - Rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta akiwa na Rais William Ruto katika Uwanja wa Michezo wa Kitaifa wa Moi at the Moi, Nairobi, Kenya, Sept. 13, 2022, katika sherehe za kuapishwa.
FILE - Rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta akiwa na Rais William Ruto katika Uwanja wa Michezo wa Kitaifa wa Moi at the Moi, Nairobi, Kenya, Sept. 13, 2022, katika sherehe za kuapishwa.

Rais Ruto kwa upande mwingine alitetea suala la uagizaji wa mahindi au chakula kilichofanyiwa mabadiliko ya kijenetiki maarufu kama GMO, ambalo limezusha upinzani mkubwa nchini mwake.

Katika mkutano huu na waandishi wa Kenya, Rais Ruto amegusia masuala mbali mbali ya uchumi maendeleo na elimu akiwahakikishia wa Kenya kwamba wanafanya kazi kuinua maisha ya wananchi.

Baadhi ya taarifa hii inatokana na shirika la habari la Reuters

XS
SM
MD
LG