China na Russia zilitumia siku ya pili ya Mkutano wa BRICS wa nchi zinazoibukia kiuchumi, kuzikosoa nchi za Magharibi, huku pia zikiunga mkono mapendekezo ya upanuzi wa kile kinachoonekana na wengine, kama kundi mbadala lenye nguvu duniani.
Viongozi wa Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini walifanya mazungumzo ya faragha Jumatano juu ya uwezekano wa upanuzi wa muungano wao wa kiuchumi wa BRICS, hatua ambayo wanasema ni njia ya kuinua sauti ya mataifa yanayoendelea, lakini ambayo pia inatumika kwa maslahi ya kisiasa ya Beijing na Moscow.