Prigozhin alikuwa ameenda Belarus kama sehemu ya makubaliano ya mwezi uliopita, ili kumaliza uasi wa muda mfupi, wa wa Juni 23, dhidi ya Rais wa Russia, Vladimir Putin, na maafisa wa ulinzi wa nchi hiyo.
Kikundi cha mamluki cha Wagner, kilikuwa kikilipwa na serikali ya Putin, kupigana pamoja na wanajeshi wa Russia nchini Ukraine, lakini mara kwa mara alilalamika kwamba Russia haikutoa silaha za kutosha kwa vikosi vyake.
Madai ya Lukashenko kwamba Prigozhin, aliyekuwa mwandani wa karibu wa Putin, alikuwa amerejea Russia, hayakuweza kuthibitishwa mara moja, na Kremlin ilikataa kutoa kauli yoyote juu ya mahali alipo Prigozhin.
Vyombo vya habari vya Russia, vimeripoti kwamba hivi karibuni, alionekana kwenye afisi zake, mjini St. Petersburg.
Rais Lukashenko alitupilia mbali mapendekezo kwamba Putin anaweza kuamuru Prigozhin auawe, akisema, "Ikiwa unafikiri kwamba Putin ni mkatili na mwenye kulipiza kisasi kummaliza, hapana, haitatokea."
Forum