Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 29, 2024 Local time: 03:31

Papa Francis awashutumu walanguzi wa dawa za kulevya


Pope Francis akihubiri kutoka Vatican, June 16, 2024. (Vatican Media/­Handout via Reuters)
Pope Francis akihubiri kutoka Vatican, June 16, 2024. (Vatican Media/­Handout via Reuters)

Papa Francis leo Jumatano aliwashutumu walanguzi wa dawa za kulevya kama "wauaji na akashutumu kulegeza sheria ya  dawa za kulevya matokeo yake ni kuongeza matumizi.

Francis alitumia somo lake lote la kila wiki la katekisimu kuzungumzia juu ya matumizi mabaya ya dawa za kulevya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Umoja wa Mataifa dhidi ya Matumizi Mabaya ya Dawa za Kulevya na Usafirishaji Haramu.

Alitoa wito wa kuongezwa kwa juhudi za kuzuia na kuwatunza waraibu, akisema tatizo la ulanguzi wa dawa za kulevya "linahitaji kitendo cha ujasiri kutoka kwa jamii yetu kwa ujumla."

Francis anajua moja kwa moja masaibu ya waraibu, baada ya kutumia miaka mingi kuwahudumia watu katika vitongoji duni vya Buenos Aires ambapo dawa ya bei nafuu "paco", iliyotengenezwa kutokana na mabaki ya kokeini, ilikuwa ikiwaharibu vijana.

Argentina kwa muda mrefu imeweka kipaumbele cha kuwatembelea waraibu wanaopona wakati wa ziara zake za nje.

Forum

XS
SM
MD
LG