Papa Francis leo Jumapili aliongoza Misa ya Pasaka kwa maelfu ya Wa-katoliki katika uwanja wa Saint Peter’s huko Vatican City kabla ya kutoa baraka zake za jadi, huku wasiwasi ukiongezeka kuhusu afya yake.
Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 87 aliwasili akiwa katika kiti cha magurudumu ili kuongoza misa hiyo kuanzia saa nne asubuhi kwa saa za huko, katika hali ya hewa ya mawingu na upepo, huku matukio hayo yakirushwa moja kwa moja kote duniani.
Papa Francis atatangaza baraka kwa Jiji na Dunia, saa za mchana ambapo anatarajiwa kuelezea migogoro ya kimataifa inayoendelea duniani kote. Jumapili ya Pasaka inaashiria kufufuka kwa Yesu Kristo, na ni kilele cha Wiki Takatifu, sehemu kubwa ya kalenda ya Ki-katoliki inayofuatiliwa na waumini bilioni 1.3.
Forum