Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 10:14

Papa Francis atoa wito wa kusitishwa kwa mauaji ya DRC


Mkuu wa kanisa Katoliki Papa Francis akihutubia umati Jumapili.Juni 16, 2024. (Vatican Media/­Handout via Reuters)
Mkuu wa kanisa Katoliki Papa Francis akihutubia umati Jumapili.Juni 16, 2024. (Vatican Media/­Handout via Reuters)

Mkuu wa kanisa Katoliki Papa Francis Jumapili ametoa wito wa kusitishwa  kwa ghasia na mauaji ya raia kwenye jimbo la Kivu Kaskazini mashariki mwa Congo.

Takriban watu 7 waliuwawa Ijumaa na Jumamosi wakati wananchi walipokuwa wakiandamana kulalamikia mauaji mabaya kutoka kwa watu wanaoshukiwa kuwa waasi wa kiislamu.

Wakati akihutubia umati kwenye bustani ya St Peter mjini Vatican, Papa Francis amesema, “Taarifa za kuhuzunisha zinaendelea kutufikia kuhusu mashambulizi na mauaji mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia jya Congo.

“Naomba mamlaka za kitaifa pamoja na jumuia ya kimataifa kufanya kila wawezalo ili kukomesha ghasia hizo na kulinda maisha ya raia. “Ameongeza kusema. Pia ametoa wito wa amani huko Ukraine, Israel, Palestina, Sudan na Myanmar, pamoja na sehemu nyingine ambako watu wanateseka kutokana na vita.

Forum

XS
SM
MD
LG