Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 12:52

Papa Francis anatarajiwa kuanza ziara DRC Jumanne, atumainiwa kuleta faraja


Papa Francis
Papa Francis

Papa Francis anaanza ziara yake huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Januari 31 kwa ujumbe wa amani na maridhiano, safari ambayo inatumainiwa kuleta  faraja  katika  nchi hiyo iliyoathiriwa  na  vita.

Kanisa Katoliki mjini Kinshasa linasema lengo la "safari ya kiuchungaji ya Papa Francis nchini Congo ni kuwakaribisha raia wa Congo, kuongeza maombi ili kuponya vidonda vya kila aina kwa njia ya kuonyesha upendo kati yao ili kukabiliana na matatizo ya nchi hiyo ambazo dalili zake zinaonekana dhahiri hivi leo.

Atakapowasili Kinshasa, mkuu wa Kanisa Katoliki atakuwa ametimiza safari yake ya 40 ya nje ya nchi tangu alipotawazwa kuwa papa.

Lakini katika ratiba yake, DRC ikiwa ni nchi ya 59 kuitembelea, ni ya kipekee sawa na Sudan Kusini ambayo ni ya 60. Atakaa Kinshasa hadi Februari 3, atakapoondoka kuelekea Juba na Askofu Mkuu wa Canterbury Justin Welby.

Kauli mbiu ya ziara yake huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo "Wote tunapatanishwa katika Yesu Kristo" na amezungumza kwa shauku kuhusu umuhimu wa kuwaachia watu wa Congo kuchagua mustkabali wa, akiwakejeli watu kutoka mataifa ya nje kwa kupora rasilimali za asili za eneo hilo wakati vita vinaendelea.

Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo … ni kama ngome, mhimili wa msisimko. Unachotakiwa tu uangalie hapa Rome katika jamii ya Wacongo” aliliambia jarida la Mundo Negro, linalotolewa na Wamishonari wa Comboni nchini uhispania, mapema mwezi wa Januari.

“Nilikuwa nikiisubiri kwa hamu safari hii, nilitamani ije haraka iwezekanavyo. Jamii ya watu wa Sudan Kusini inateseka (hata) Congo inateseka katika kipindi hiki kwa sababu ya vita, ndiyo maana sitakwenda Goma, kwa kuwa siyo rahisi kwa sababu ya mapigano. Siyo kwamba siendi kwasababu naogopa , lakini hali ni tete na kuona kile kinachotokea .. lazima tuwajali watu.”

Ziara ya awali ya papa Francis katika nchi hizo mbili ilikuwa Julai mwaka 2022, iliahirishwa kutokana na tatizo la goti. Sasa ni wakati mzuri zaidi. Baba mtakatifu hivi sasa anakwenda katika eneo hilo huku mivutano ikiwa juu kati ya DRC na jirani yake Rwanda kuhusu ukiukaji wa usalama na shutuma za kuyaunga mkono makundi yenye silaha yenye uhasama na serikali zote mbili.

Chanzo cha habari hii ni gazeti la "The East African" linalochapishwa Kenya.

XS
SM
MD
LG