Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 10:31

Papa Francis afanya mageuzi ya usawa wa kijinsia katika kanisa


Papa Francis alipokuwa katika jiji la Kinshasa huko DRC, tarehe 1 Februari 2023. Picha na Vatican Media/Handout kupitia shirika la habari la REUTERS
Papa Francis alipokuwa katika jiji la Kinshasa huko DRC, tarehe 1 Februari 2023. Picha na Vatican Media/Handout kupitia shirika la habari la REUTERS

Papa Francis ameamua kuwapa wanawake haki ya kupiga kura katika mkutano ujao wa maaskofu, mageuzi ya kihistoria ambayo yanaonyesha matumaini yake ya kuwapa wanawake majukumu makubwa ya kufanya maamuzi na kuwapa watu wa watu wa kawaida sauti zaidi katika maisha ya Kanisa Katoliki.

Francis aliidhinisha mabadiliko hayo ya kanuni zinazosimamia Sinodi ya Maaskofu, chombo cha Vatican kinacho wajumuisha Maaskofu kutoka semehu mbalimbali duniani katika mkutano mikutano ya mara kwa mara, hii inakufuatia miaka mingi ya madai ya wanawake ya kuwa na haki ya kupiga kura.

Vatikani siku ya Jumatano ilichapisha marekebisho aliyoyaidhinisha, ambayo yanasisitiza maono yake kwa waamini kuchukua jukumu kubwa katika masuala ya kanisa ambayo kwa muda mrefu yamekuwa yakifanywa na makasisi, maaskofu na makadinali.

Makundi ya wanawake wa kikatoliki ambayo kwa muda mrefu yamekuwa yakiikosoa Vatikani kwa kuwachukulia wanawake kama raia wa daraja la pili , kwa haraka makundi hayo yaliipongeza hatua hiyo ya kihistoria katika kanisa hilo.

Tangu baraza kuu wa Pili la Vatikani, katika mkutano iloiyofanyika miaka ya 1960 iliyotaka kanisa liwe la kisasa, kila wakati mapapa walikuwa wakiwaita maaskofu kutoka sehemu mbalimbali ulimwenguni kwenda Roma kwa wiki chache kwa wakati mmoja ili kujadili mada maalumu. Baada ya mkutano kumalizika, maaskofu hupiga kura juu ya mapendekezo hayo maalum na kuyapeleka kwa papa, ambaye kisha hutoa hati inayozingatia maoni yao.

Hadi sasa, watu pekee walioweza kupiga kura ni wanaume.

Lakini chini ya mabadiliko hayo mapya, masista watano wa kidini wataungana na makasisi watano kama wawakilishi wa kupiga kura kwa ajili ya maagizo hayo ya kidini.

XS
SM
MD
LG