Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 05:57

Papa Francis aombea amani kwa watu wa Ukraine, awataka Waisraeli na Wapalestina kuaminiana


Papa Francis wakati wa misa ya Pasaka, Vatican, Aprili 9. 2023.
Papa Francis wakati wa misa ya Pasaka, Vatican, Aprili 9. 2023.

Katika ujumbe wa Pasaka unaoangazia matumaini, Papa Fraancis Jana Jumapili aliwasilisha maombi kwa ajili ya watu wa Ukraine na Russia, aliyapongeza mataifa ambayo yanawakaribisha wakimbizi.

Amewataka Waisraeli na Wapalestina wanaoukumbwa na ongezeko la hivi karibuni la ghasia mbaya kujenga “hali ya kuaminiana.”

Francis, pamoja na maskofu kadhaa na maelfu ya waumini, walisherekea misa ya Pasaka katika uwanja wa Mtakatifu Petro uliopambwa kwa maua, wakithibitisha imani ya Kikristo kwamba Yesu alifufuka kutoka kwa wafu siku chache baada ya kusulubiwa kwake.

Papa mwenye umri wa miaka 86, aliongoza sherehe kwa hotuba ya kawaida kuhusu maeneo yenye matatizo duniani.

Akihimiza “kuaminiana kati ya watu, watu na mataifa, “ Francis alisema furaha ya Pasaka inaangazia giza.

Wanadiplomasia wa Ukraine wamekuwa wakilalamika kwamba hajatoa msimamo thabiti katika taarifa zake juu ya Russia na hasa Vladimir Putin wakati Vatican inajaribu kuepuka kuitenga Moscow.

“Wasaidie wapendwa watu wa Ukraine katika safari yao ya kuelekea kwenye amani na uwape mwanga wa pasaka watu wa Russia,” Francis alimuomba Mungu katika hotuba yake ya Pasaka, aliyoitoa akiwa amekaa kwenye kiti kwenye roshani ya Kanisa ya Mtakatifu Petro.

XS
SM
MD
LG