Baada ya wiki moja ya mazungumzo mjini Jeddah, Saudi Arabia, jeshi la Sudan na kikosi cha RSF wametia saini makubaliano ya kufanya kazi kuelekea katika sitisho fupi la mapigano kwa majadiliano zaidi, wamesema.
Waraka wa makubaliano uliotolewa baada ya mazungumzo umesema pande hizo mbili zimeweka nia ya dhati ya kuweka kipaumbele kwa majadiliano ya kufanikisha sitisho la muda mfupi la mapigano ili kufanikisha upelekaji wa misaada ya dharura ya kibinadamu na kurudisha huduma muhimu.
Taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema pande hizo mbili zitazingatia zaidi kufikia makubaliano ya sitisho la mapigano litakalofanya kazi kwa kiasi cha siku kumi.
Wapatanishi wanafanya kazi na Saudi arabia na marekani wanaosimamia majadiliano hayo baadaye watazungumzia hatua maalumu za usalama kwa ajili ya ulinzi wa vifaa vya misaada, afisa wa Marekani amesema.
Hata hivyo Washington inategemea pande hizo mbili kukubali kutia saini makubaliano hayo kutajenga nguvu zaidi .