Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 18:28

Ongezeko la ghasia laibua wasiwasi mkubwa Equador


Maafisa wa usalama nchini Equador.
Maafisa wa usalama nchini Equador.

Rais wa Ecuador Daniel Noboa alisema Jumanne kuwa nchi yake iko katika hali ya "mgogoro wa silaha" huku kukiwa na ongezeko la ghasia katika taifa hilo la Amerika ya Kusini.

Rais huyo alitoa tamko hilo saa chache baada ya kundi la watu waliojifunika nyuso zao wakiwa na bunduki na vilipuzi, kuvamia kituo cha televisheni cha umma katika mji wa bandari wa Guayaquil, wakati wa kipindi cha habari cha moja kwa moja, na kufyatua risasi ndani ya studio.

Baadaye polisi walichukua udhibiti wa kituo hicho na kuwakamata washukia 13 na kuwafungulia mashtaka ya ugaidi. Hakuna aliyejeruhiwa katika tukio hilo.

Mgogoro huo ulianza mwishoni mwa juma kwa kutoroka kwa Adolfo Macias, kiongozi wa genge la ulanguzi wa dawa za kulevya la Los Choneros. Kakiaka miaka ya karibuni, maafisa kadhaa wa polisi wametekwa nyara na mabomu mengi yamelipuliwa kote Ecuador.

Mamlaka Jumanne zilisema kiongozi mwingine wa kundi la ulanguzi wa dawa za kulevya, la Los Lobos, Fabricio Colon Pico, alitoroka kutoka mikononi mwa polisi kutoka mji wa Riobamba. Colon Pico ameshutumiwa kwa kuhusika katika njama ya kumuua mwanasheria mkuu wa nchi hiyo.

Rais Noboa alitangaza hali ya hatari Jumatatu kujibu ghasia hizo. Mbali na tangazo la Jumanne la nchi kuwa chini ya "mgogoro wa wa silaha," Noboa alitaja zaidi ya magenge 20 ya ulanguzi wa dawa za kulevya kuwa mashirika ya kigaidi na kuyatangaza kuwa malengo ya kijeshi.

Forum

XS
SM
MD
LG