Kitakachotokea katika miezi ijayo kinaweza kubadilisha mizani ya dunia katika mwelekeo wa demokrasia au utawala wa mabavu. Hivi ndiyo chaguzi kuu katika nchi sita muhimu zitakazofanyika baadaye mwaka huu zitakavyokuwa na mchango katika maeneo ambayo yamekuwa na mzozo kwa muda mrefu.
Kuanzia mwishoni mwa karne ya 19, na katika kipindi cha vita mbili za dunia, sera ya mambo ya nje ya Marekani imepitia mtikisiko wa madadiliko kutoka sera za kujitenga na kuanza kujihusisha katika utengenezaji wa utaratibu wa dunia.
Ni muhimu kuelewa tofauti zilizopo kati ya mitazamo hiyo ya kidunia, waziri mdogo wa zamani wa ulinzi wa marekani Joseph S. Nye Jr. aliiambia Sauti ya Amerika, kwa sababu ajenda ya kwanza ya rais wa zamani wa Marekani Donald Trump ni kuitaka kuifanya Marekani ijitenge tena.
Hiyo itawaacha washirika wa Marekani wakisuasua wakati mivutano ikiongezeka kati ya Taiwan na China, na Russia-Ukraine na vita kali vya Israel- Hamas.
Kuna uwezekano Trump huenda akawa mgombea wa chama cha Republican, amekuwa akiishambulia NATO mara kwa mara, mshirika muhimu wa kijeshi wa Marekani, na haijachukua msimamo thabiti wa jinsi gani, au kama itaiunga mkono Israel katika vita yake dhidi ya Hamas endapo Hamas itachaguliwa tena.
Kwa upande mwingine, Rais aliyeko madarakani wa chama cha Democratic Joe Biden ambaye ukusanyaji maoni unaonyesha kuwa ni mgombea atakaye chuana na Trump, amepeleka misaada ya kijeshi Kyiv na Jerusalem hata wakati akipata shinikizo kutoka kwa wabunge wa Republican kuhusu maendeleo machache huko Ukraine na kutoka kwa wapenda maendeleo juu ya kusambaa kwa mzozo wa kibinaadamu huko Gaza.
Wagombe hao wawili wa urais wanaoongoza, ni wazi wameonyesha mitazamo tofauti ya Marekani duniani, atakayeshinda Novemba atafanya maamuzi ya jinsi Marekani itakavyokuwa mkali kwa China, Russia na washindani wengine wakimataifa.
Kufuatia uvamizi wa Russia huko Ukraine takribani miaka miwili iliyopita, washirika wa Kyiv wameifanya Russia kuwa nchi iliyowekewa vikwazo zaidi duniani, kuuvuruga uchumi wake na kuisukuma karibu na Beijing, ambayo sasa ni mfanyabiashara mkubwa.
Mbali na ongezeko la mfumuko wa bei, wachambuzi hawatajii Rais wa Russia Vladimir Putin kuondolewa madarakani mwaka 2024, huku wapinzani wake wakubwa wa kisiasa wakifungwa, kufukuzwa, kutoweka au kuuawa katika mazingira ya kutatanisha.
huku wapinzani wake wakubwa wa kisiasa wakifungwa, kufukuzwa, kutoweka au kuuawa chini ya hali ya kutisha.
mfumuko wa bei unaoongezeka
Nchi nyingine zinazotarajiwa kufanya uchaguzi mwaka huu ni pamoja na Taiwani, Umoja wa Ulaya, India na Afrika Kusini.
Forum