Mahakama hiyo imesema uamuzi huo ni kutokana na ushiriki wa Trump, katika kubadilisha matokeo ya uchaguzi wa rais wa mwaka 2020.
Uamuzi huo umesimamishwa baada ya kuwasilishwa kwa rufaa katika mahakama ya juu ya Marekani, lakini haujazuia wengi ndani ya chama ikijumuisha baadhi ya wapinzani wa rais huyo wa zamani kujadili uamuzi huo na kusema si wa kidemokrasia na majaribio ya kuondoa uamuzi wa kuchagua mgombea urais wa Republikan mikononi mwa wapiga kura.
Kutokana na ugombea wa Trump, kuwekewa pingamizi na zaidi ya dazeni ya majimbo, mwenyekiti wa Republikan, Ronna McDaniel, ametumia mtandao wa kijamii wa X kutokubaliana na uamuzi na kudai ni kuingilia mambo ya uchaguzi wa chama.
Forum