Katibu wa masuala ya ndani ya jimbo la Maine katika chama cha Democratic aliondoa jina la rais wa zamani Donald Trump katika karatasi ya uchaguzi wa rais wa jimbo hilo chini ya kifungu cha katiba ya Marekani kwenye kipengele kinachoelezea uasi na kuwa afisa wa kwanza wa uchaguzi kuchukua hatua iliyofanywa na upande mmoja katika uamuzi ambayo kuna uwezekano wa kuleta madhara katika Kura za Wajumbe.
Wakati jimbo la Maine lina kura nne tu za uchaguzi ni moja ya majimbo mawili yanayogawana kura hizo. Trump alishinda kura moja ya Maine mwaka 2020 kwa hivyo kuondoa jina lake kwenye sanduku la kura iwapo ataibuka kuwa mgombea wa chama cha Republican inaweza kuwa na athari kubwa katika kinyang'anyiro ambacho kinatarajiwa kuamuliwa na wachache.
Uamuzi huo wa kiongozi wa masuala ya ndani wa Maine, Shenna Bellows unafuatia uamuzi wa Disemba wa Mahakama ya Juu ya jimbo la Colorado ambapo ilimuondoa Trump katika sanduku la kura chini ya kifungu cha 3 cha kipengele cha 14 cha katiba ya Marekani.
Colorado ni jimbo linaloongozwa na chama cha Democratic ambalo halitarajiwi kuwa na ushindani kwa Warepublican mwezi Novemba. Bellows aligundua kuwa Trump hakuweza tena kugombea nafasi yake ya awali kwa sababu ya jukumu lake katika shambulio la Januari 6, mwaka 2021 dhidi ya jengo la bunge la Marekani lilikiuka kifungu cha 3 ambacho kinapiga marufuku kwa wale waliopo ofisini “waliojihusisha na uasi”.
Bellows alitoa uamuzi huo baada ya baadhi ya wakaazi wa majimbo ikijumuisha pamoja kundi la wabunge wa zamani waliompa changamoto Trump juu ya jina lake kuwepo katika sanduku la kupiga kura.
Forum