Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 06:02

Edorgan ateuwa waziri wa zamani kuwania wadhifa wa Meya wa Istanbul kupitia chama tawala


Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan Jumapili amemteua waziri wa zamani wa mazingira Murat Kurum kuwa mgombea wa chama chake ya AKP kwenye uchaguzi wa Meya wa Istanbul, utakaofanyika Machi, ikiwa kama juhudi ya kurejesha udhibiti wa mji huo mkuu.

Kurum atamenyana na meya wa sasa Ekrem Imamoglu kutoka chama kikuu cha upinzani cha Republican People’s CHP ambaye ushindi wake wa kiti hicho 2019, ulifikisha kikomo utawala wa miaka 25 wa chama tawala cha AKP mjini humo.

Mei mwaka 2023, Edorgan alishinda urais kwa muhula mwingine wakati chama chake cha APK pamoja na vyama shirika wakichukua wingi wa viti bungeni, ikiashiria changamoto iliyopo kwa upinzani kwenye viti vya manispaa kote nchini kwenye uchaguzi wa Machi 31.

Kurum mwenye umri wa miaka 47 alikuwa waziri wa mazingira na miji kuanzia Julai 2018 hadi Juni mwaka jana, alipoacha wadhifa huo baada ya uchaguzi, pale alipochaguliwa kama mbunge wa Istanbul. Mji huo ndio wa kibiashara nchini Uturuki, ukiwa na wakazi milioni 16 ambao ni sawa na asilimi 20 ya wakazi nchini humo.

Kurum alikuwa mmoja wa viongozi wakuu serikalini waliochangia pakubwa baada ya mkasa wa tetemeko la ardhi kusini mwa Uturuki Febuari mwaka jana, lililouwa zaidi ya watu 50,000.

Forum

XS
SM
MD
LG