Mjumbe maalum wa mataifa ya ASEAN amekutana na kiongozi wa kijeshi wa Myanmar katika juhudi za hivi karibuni za kutaka kuanzisha mazungumzo kati ya jeshi na viongozi wanaopinga mapinduzi hayo, pamoja na suala la kufanyika msako mkali wenye umwagikaji wa damu.
Muungano wa mataifa yaliyo kusini mwa Asia, umeongeza juhudi za kidiplomasia zilizokwama, kujaribu kumaliza mgogoro uliosababishwa na mapinduzi ya mwaka uliopita dhidi ya utawala wa Aung San Suu Kyi, na kupelekea maandamano makubwa.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Cambodia Prak Sokhonn na kiongozi wa mapinduzi Min Aung Hlaing, wamezungumzia hali ya maandamano na machafuko kutokana na mgogoro huo wa kisiasa, pamoja na namna ya kushirikiana kwa ajili ya kufikisha msaada wa kibinadamu.
Ziara ya mjumbe huyo maalum, itakayomalizika Jumatano, inalenga kuhakikisha Kamba kuna ushauriano wa kisiasa kati ya wahusika wote.
Habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali vya habari.