Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 20:38

Mwandishi wa habari wa Marekani Fenster aachiliwa huru Myanmar


Danny Fenster
Danny Fenster

Mwandishi wa Habari wa Marekani Danny Fenster ameachiliwa kutoka jela huko Myanmar.

Kuachiliwa huko kumetokea siku tatu baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 11 kwa kile ambacho Yangon imesema ni kutokana na kukiuka sheria za uhamiaji na ugaidi.

Hayo yamethibitishwa na waajiri wake na balozi wa zamani wa Marekani katika Umoja wa Mataifa.

Balozi huyo wa zamani wa Marekani katika UN Bill Richardson alisema Jumatatu kwamba Fenster amekabidhiwa kwake huko Myanmar na hivi karibuni atakuwa njiani kurejea nyumbani akipitia Qatar.

” Hii ni siku ambayo unatarajia itafika wakati ukifanya kazi hii,” alisema Richardson.

Ameongeza, "Tunashukuru sana Danny hatimaye ataweza kuungana tena na wapendwa wake ambao wamekuwa wakimtetea wakati huu wote dhidi ya vikwazo mbali mbali."

Gazeti la Frontier Myanamar ambalo Fenster amekuwa akifanyia kazi kabla ya kukamatwa kwake pia limethibitisha kuachiliwa kwake.

Wakati huohuo chanzo cha Habari cha serikali kimeliambia shirika la Habari la AFP kwamba Fenster amepelekwa katika mji mkuu NAYIPIDA kutoka Yangon na atasafirishwa kuondoka nchini.

Habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali vya habari

XS
SM
MD
LG