Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 06:26

Mwenyekiti wa BBC ajiuzulu


Mwenyekiti wa BBC Richard Sharp akitoa ushahidi mbele ya Kamati ya Dijitali, Utamaduni, Vyombo vya Habari na Michezo (DCMS) huko London. Picha na Kitini / PRU / AFP .
Mwenyekiti wa BBC Richard Sharp akitoa ushahidi mbele ya Kamati ya Dijitali, Utamaduni, Vyombo vya Habari na Michezo (DCMS) huko London. Picha na Kitini / PRU / AFP .

Mwenyekiti wa shirika la utangazaji la BBC Richard Sharp alijiuzulu Ijumaa baada ya ripoti huru kubaini kuwa alikiuka kanuni kuhusiana na mkopo wa dola milioni moja aliochukua waziri mkuu wa zamani wa Uingereza, Boris Johnson, akiwa madarakani.

Kuondoka kwake madarakani kunakuja wakati wa uchunguzi wa kisiasa katika shirika hilo la utangazaji la Uingereza. Mzozo wa mkubwa sana unaomhusu mtangazaji ayelipwa mshahara mkubwa zaidi Gary Lineker, katika mzozo huo wa kutoegemea upande wowote ulitawala vichwa vya habari nchini Uingereza mwezi uliopita.

Sharp, ambaye aliwahi kufanya kazi katika benki ya Goldman Sachs alichukua nafasi ya mwenyekiti wa BBC mwaka 2021, alikuwa katika shinikizo tangu mwezi Februari wakati kamati ya wabunge iliposema kuwa alifanya "makosa makubwa katika maamuzi" kwa kushindwa kutangaza kuhusika kwake katika mkopo huo.

Sharp alisema amekubali kuendelea kuwepo kazini hadi mwisho wa Juni ili kuipa serikali muda wa kupata mtu mwingine atakae ongoza shirika hilo la utangazaji, linalohifadhiliwa na ada ya leseni inayolipwa na kaya zinazotazama televisheni.

Uchunguzi huo, ulioanzishwa na shirika la uangalizi wa uteuzi wa umma, ulimchunguza Sharp ambaye alichaguliwa na serikali kuwa mwenyekiti wa shirika hilo mnamo 2021.

Hususani waliangalia endapo Sharp aliweka wazi kama ilivyotakiwa maelezo kuhusu jukumu lake katika kuwezesha upatikanaji wa mkopo wa dola milioni moja kwa Johnson kabla ya kuteuliwa kuwa mwenyekiti.

Ripoti hiyo iligundua kuwa, wakati alipokiuka kanuni za serikali kuhusu uteuzi wa umma, ukiukaji huo si lazima ubatilishe uteuzi wake. Sharp alisema aliamini kuwa ukiukaji huo ulifanyika "bila kukusudia na siyo muhimu."


Msemaji wa masuala ya utamaduni wa chama cha upinzani cha Labour, Lucy Powell, alisema ukiukaji huo "umesababisha uharibifu mkubwa wa sifa ya shirika hilo la BBC na kudhoofisha uhuru wake kutokana na upendeleo na ukosefu wa maadili wa chama cha Conservative.

XS
SM
MD
LG