Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:03

Biden akutana na Rais wa Ireland huko Phoenix Park


Rais wa Marekani Joe Biden akiwa Ireland ya Kaskazini.
Rais wa Marekani Joe Biden akiwa Ireland ya Kaskazini.

Rais wa Marekani Joe Biden amekutana na rais wa Ireland Michael D. Higgins leo Alhamisi.

Rais wa Ireland Michael D. Higgins. Reuters/Jason Cairnduff
Rais wa Ireland Michael D. Higgins. Reuters/Jason Cairnduff

Biden alilakiwa na Higgins na mkewe wakati alipowasili katika makazi rasmi ya rais wa Ireland.

Wakati wa ziara yake Biden anatarajiwa kupiga kengele ya amani iliyozinduliwa mwaka 2008 kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 10 ya mkataba wa ijumaa kuu ambao ulimaliza miongo kadhaa ya vurugu huko Ireland kaskazini.

Pia anatarajiwa kushiriki katika hafla ya upandaji wa mti ukiwa karibu na ule uliopandwa na rais wa zamani wa marekani Barack Obama.

Siku ya Jumatano Rais wa Marekani Joe Biden alikutana na Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak mjini Belfast, Ireland Kaskazini leo kama sehemu ya kuadhimisha miaka 25 ya makubaliano ya amani ya mwaka 1998 ya Ireland kaskazini.

Rais wa Marekani Joe Biden akiwa na Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak walipokutana katika Hoteli ya Grand Central, Belfast, Ireland ya Kaskazini April 12, 2023. REUTERS/Kevin Lamarque
Rais wa Marekani Joe Biden akiwa na Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak walipokutana katika Hoteli ya Grand Central, Belfast, Ireland ya Kaskazini April 12, 2023. REUTERS/Kevin Lamarque

Biden anayejivunia sana asili yake ya Ireland atatumia zaidi ya nusu siku katika eneo la Uingereza kabla ya kusafiri kwenda kusini katika jamhuri ya Irelanda kwa siku mbili na nusu za hotuba na mikutano na maafisa na kukutana na ndugu wa mbali.

Kusimama kwake kwa muda mfupi mjini Belfast kunakuja huku kukiwa na kukwama kwa kisiasa hivi karibuni ambao ulihusu kushirikiana madaraka, kiini cha mkataba wa amani wa mwaka 1998, hatua ambayo haijtekelezwa kwa zaidi ya mwaka mmoja kutokana na mzozo kuhusu mipango ya biashara baada ya Brexit.

Kuondoka kwa Uingereza katika Umoja wa ulaya kwa kiasi Fulani kuliharibu uhusiano kati ya uingereza na ikulu ya Marekani , wakati London na brussels zikihangaika kutafuta makubaliano ya kuachana ambayo hayataharibu kanuni za makubaliano ya amani.

Makubaliano ya Good Friday – ambayo Marekani ilisaidia kufikiwa Aprili 10, 1998 – yalimaliza kwa kiasi kikubwa miongo kadhaa ya ghasia za madhehebu ambazo ziliigubika Ireland Kaskazini tangu mwishoni mwa miaka ya 1960 na pia zilisababisha mashambulizi ya mara kwa mara kwa Uingereza bara. Wakati bado kuna ghasia za hapa na pale huko Ireland Kaskazini, mkataba huo ulikiwezesha kizazi cha watoto kukulia katika mazingira ya amani.

XS
SM
MD
LG