Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 14, 2025 Local time: 01:38

Mwandishi wa vitabu wa Uganda Kakwenza Rukirabashaija aachiliwa - CCG


 Kakwenza Rukirabashaija (Twitter/@KakwenzaRukira)
Kakwenza Rukirabashaija (Twitter/@KakwenzaRukira)

Mwandishi wa riwaya Kakwenza Rukirabashaija ameachiliwa huru, waangalizi wa katiba wametoa taarifa.

Mtunzi wa vitabu wa Uganda Rukirabashaija aliachiliwa asubuhi ya Jumatano na amepelekwa kufanyiwa uchunguzi wa afya yake,” kituo cha Uongozi wa Katiba (CCG) kimesema katika taarifa yake fupi katika mtandao wa Twitter Jumatano.

Mwanaharakati huyo mwenye umri wa miaka 33 alipewa dhamana kutokana na sababu za kiafya na kuachiliwa kutoka katika gereza la Kitalya, mjini Kampala Jumanne.

Lakini muda mfupi baada ya kutoka nje ya gereza, alichukuliwa na wanaodhaniwa kuwa ni maafisa wa usalama na kumlazimisha kupanda gari yenye vioo visivyo ruhusu kuona ndani ammbayo haikuwa na namba ya usajili. Gari hilo baadae liliondoka kwa kasi, kwa mujibu wa wakili wake Erin Kiiza.

Mapema jana Umoja wa Ulaya uliwakosoa vikali maafisa wa usalama wa Uganda kwa kumkamata tena mwandishi wa Riwaya Rukirabashaija muda mfupi baada ya mahakama kuamuru aachiliwe kwa dhamana.

Taarifa ya umoja wa ulaya imeeleza hatua hiyo ni kutoheshimu utawala wa sheria na kutoa wito kuachiliwa haraka kwa bwana Rukirabashaija. Alikamatwa desemba baada ya kutoa matamshi yasiyofurahisha kuhusu rais Yoweri Museveni na mwanawe kwenye mitandao ya kijamii.

Mwaka 2020 mwandishi huyo alihojiwa ikiwa kitabu chake The Greedy Barbarian kilimhusu bwana Museveni, anasema aliteswa akiwa kizuizini.

XS
SM
MD
LG